Sunday, 1 May 2016

WALIO KUWA WAFANYAKAZI WA CLOUDS FM ..Gerald Hando na PJ waanza kazi EFM kwa mkwara huu.

 Gerald Hando, Adella Tillya na Paul James wakiwa nje ya jengo la K-Net wakiendesha kipindi chao live
 
Kwa siku nyingi wapenzi wa redio walikuwa wakiwasubiri kwa hamu Gerald Hando na Paul James waliohamia EFM kuona wana kipya gani.

Leo, May 2, wawili hao wameanza kwenda hewani kupitia kipindi cha Joto la Asubuhi. Aliyekuwa mtayarishaji wa kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM walikokuwa wawili hao, Abel Onesmo naye ameungana nao.

0 comments:

Post a Comment