Saturday 16 July 2016

#BURUDANI>>>TUTAPAMBANA NA WALE WOTE WANAOJIHUSISHA NA WIZI WA KAZI ZA WASANII NA WANAOZISAMBAZA KINYUMBE CHA SHERIA:WAZIRI NAPE.Fahamu zaidi hapa.

 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na Mkurugenzi wa Steps Entertainment Bw. Delish Solanki wakati akiwasili katika ukumbi wa Suncrest Cine Plex uliopo katika jengo la Quality Centre Jijini Dar es Salaam kuzindua filamu ya Sikitu Julai 15, 2016.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ameahidi kupambana na wale wote wanaojihusisha na wizi wa kazi za wasanii na kuzisambaza kinyume cha sheria.
Mhe. Nape Nnauye ametoa ahadi hiyo mbele ya wasanii na wadau wa sanaa wakati akizundua filamu ya Sikitu na kuahidi kutochoka kupambana katika vita dhidi ya wezi wa kazi za wasanii wa filamu na sanaa kwa ujumla.“Nataka niwahakikishie wasanii na watengeneza filamu Tanzania kazi hii nimeianza na nitaendelea nayo na hatutoshindwa tutashinda na nawaonya wanaofanya kazi ya kuiba kazi za wasanii waache mara moja” alisema Mhe. Nnauye.

Mhe. Nnauye ameongeza kuwa Serikali itaendelea kujenga misingi mizuri kwa wasanii na tasnia ya filamu Tanzania na kuhakikisha wasanii na watayarishaji wanapata mitaji itakayowawezesha kuzalisha filamu bora na kupata masoko mazuri.Aidha amewaomba wadau wa sanaa na filamu kwa ujumla kukaa na Serikali na kuangalia namna bora ya kurasimisha vibanda vinavyoonesha filamu za kitanzania kuwa kumbi maalum kwa ajili ya kuonesha filamu hizo ili kuongeza soko la filamu hizo kupitia kumbi hizo.

Kwa upande wake katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo amewapongeza watayarishaji wa filamu hiyo kwa kuzingatia maadili na wazidi kutengeneza filamu zenye ubora zaidi ili kukuza tasnia ya filamu nchini.

Filamu ya Sikitu imetayarishwa na kutengenezwa na Kajala Entertainment na imehusisha wasanii wengi wenye uwezo mkubwa akiwemo Taiya, Mutrah, Jada, Asha Boko, Hemed Suleimani, kajala Masanja, Amir Athuman ‘King Majuto’ na wengine wengi, imeandikwa na kuongozwa na Leah Richard Mwendamseke na itaoneshwa katika kumbi za sinema kwa muda wa siku saba kabla ya kuingia sokoni.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Suncrest Cine Plex uliopo katika jengo la Quality Centre Jijini Dar es Salaam kuzindua filamu ya Sikitu Julai 15, 2016.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na muigizaji mkongwe nchini na mmoja ya waigizaji katika filamu ya Sikitu Amir Athumani ‘King Majuto” wakati akiwasili katika ukumbi wa Suncrest Cine Plex uliopo katika jengo la Quality Centre Jijini Dar es Salaam kuzindua filamu ya Sikitu Julai 15, 2016.
 Mkurugenzi wa Steps Entertainment Bw. Delish Solanki akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akiwasili katika uzinduzi wa filamu ya Sikitu katika ukumbi wa Suncrest Cine Plex uliopo katika jengo la Quality Centre Jijini Dar es Salaam Julai 15, 2016.
 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi . Joyce Fisso akizungumza na wasanii na wadau wa sanaa na kumkaribisha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (hayupo pichani) kuzindua filamu ya Sikitu iliyooneshwa kwa mara ya kwanza katika ukumbi wa Suncrest Cine Plex uliopo katika jengo la Quality Centre Jijini Dar es Salaam Julai 15, 2016.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na wasanii na wadau wa sanaa wakati wa uzinduzi wa filamu ya Sikitu katika ukumbi wa Suncrest Cine Plex uliopo katika jengo la Quality Centre Jijini Dar es Salaam Julai 15, 2016.
 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi . Joyce Fisso akijadiliana jambo na mmoja ya waigizaji katika filamu ya Sikitu Bi. Tausi Mdegela kabla ya uzinduzi wa filamu hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Suncrest Cine Plex uliopo katika jengo la Quality Centre Jijini Dar es Salaam Julai 15, 2016.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (wa pili kulia) akifatilia filamu ya Sikitu aliyoizinduwa na kuoneshwa kwa mara ya katika ukumbi wa Suncrest Cine Plex uliopo katika jengo la Quality Centre Jijini Dar es Salaam Julai 15, 2016 Kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi . Joyce Fisso, wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Steps Entertainment Bw. Delish Solanki na kushoto ni muigizaji mkongwe nchini na mmoja ya waigizaji katika filamu hiyo Amir Athumani ‘King Majuto”
  Mtayarishaji na muigizaji katika Filamu ya Sikitu, Kajala Masanja akifurahia filamu hiyo iliyozinduliwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye na kuoneshwa kwa mara ya kwanza katika ukumbi wa Suncrest Cine Plex uliopo katika jengo la Quality Centre Jijini Dar es Salaam Julai 15, 2016
Muigizaji mkongwe nchini na mmoja ya waigizaji katika filamu ya Sikitu, Amir Athumani ‘King Majuto”( kushoto) akifatilia filamu hiyo iliyozinduliwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye na kuoneshwa kwa mara ya kwanza katika katika ukumbi wa Suncrest Cine Plex uliopo katika jengo la Quality Centre Jijini Dar es Salaam Julai 15, 2016 kulia ni Mkurugenzi wa Steps Entertainment Bw. Delish Solanki.
Baadhi ya wadau wa sanaa na wananchi wakifatilia filamu ya Sikitu iliyozinduliwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye na kuoneshwa kwa mara ya kwanza katika katika ukumbi wa Suncrest Cine Plex uliopo katika jengo la Quality Centre Jijini Dar es Salaam Julai 15, 2016.

0 comments:

Post a Comment