JESHI
la Polisi nchini kwa kishirikiana na Ofisi za Interpol Kanda ya Kusini
Mwa Afrika imefanya operesheni na kukamata vipande vya meno ya Tembo
666 vyenye uzito wa Kilogram 1279.19 vyenye thamani zaidi ya Sh. Biloni
Nne.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kamishna wa
Jeshi la Polisi (CP), Diwani Athuman wakati akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam leo.Amesema kuwa vipande hivyo vya tembo vimehusisha watu tisa kati yao mmoja ni Raia wa Guinea na mwingine ni Raia wa Uganda.
Amesema
kuwa katika operesheni Usalama III wameweza kukamata vitu mbalimbali
kutokana na taarifa za kiitelijensia zilizokusanywa wakati wa
matayarisho ya operesheni ya Usalama III, ambapo waliweza kukamata
mitambo 18 ya kutengenezea gongo pamoja na lita za gongo 960
zimekamatwa.
Athuman amesema katika Operesheni hiyo wameweza kukamata watuhumiwa 265 ambapo baada ya uchunguzi watakaobainika kuhusika na vitendo vya kihalifu watafikishwa mahakamani mara moja
Kamishina
Othman amesema ametoa rai kwa wanunuzi wa magari nje ya nchi
kuwasiliana na ofisi za Interpol za ndani au nje ya nchi magari
yanakotoka kwa uchunguzi kabla ya kuyanunua ili kuondoa usumbufu wa
kukamatwa mara kwa mara katika operesheni kama hizi.
Amesema
kutokana na operesheni hiyo jeshi la polisi halitakubali kuona kundi la
watu wachache linalotishia usalama wa maisha ya raia wema na mali zao
na wataobainika kufanya hivyo watachukuliwa hatua za kisheria bila kusita.
0 comments:
Post a Comment