Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KIKOSI cha timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka
17‘Serengeti Boys’ kimefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa goli 6-0
dhidi ya timu ya Shelisheli na Ushindi huo unaifanya Serengeti kuwa na
jumla ya goli 9-0 baada ya kushinda mchezo wa awali uliopigwa katika
uwanja wa Taifa na baada ya kushinda mchezo huo wa kuwania kucheza
Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika sasa Serengeti itavaana na timu ya
Taifa ya Afrika Kusini mwezi ujao.
Mchezo ulianza kwa timu zote kushambuliana lakini Serengeti
ilionekana kuutawala mchezo huo kwa asilimia kubwa huku Timu hiyo ambayo
ni wawakilishi pekee wa nchi kwenye mashindano ya kimataifa ilipata
goli lake la kwanza dakika ya tisa kupitia kwa Ibrahim Abdallah baada ya
golikipa kutema shuti lililopigwa na Asadi Ally.
Serengeti inapata goli la pili lililofungwa na Mohemmed
Abdallah dakika ya 43 pale alipoachia shuti kali lililomshinda kipa wa
wapinzani wao na kuzama wavuni. Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika
serengeti walikuwa kifua mbele kwa goli 2 huku wakionekana kuutawala
vilivyo mchezo huo wa ugenini.
Kipindi cha pili kinaanza kwa Serengeti kuingia kwa kasi
ambayo inazaa matunda dakika ya 50 pale Asad Juma anapoandika goli la 3
baada ya kupiga faulo inayotumbukia moja kwa moja wavuni.Wageni hao
katika uwanja wa Stade Linite wanapata goli la 4 kwa penati dakika ya
61 inayopigwa na Issa Makamba na Asad Juma anaandika bao la tano dakika
ya 70 huku Yohana Mkomola akiandika goli la sita dakika ya 90
Kikosi cha Serengeti Boys
Ramadhani Kambwili
Israel Mwenda
Nickson Kibabage
Enrick Nkosi
Ally Msengi
Ally Ng’anzi
Mohameed Abdallah
Shaban Ada
Ibrahim Ally
Rashid Chambo
Asad Juma
Kikosi cha Shelisheli.
Gino Pusureuse
Juninno Mathiot
Stan Estner
Brandon Molle
Mathew Basset
Churtill Rose
Emmanuel Lesperance
Julius Joseph
Ryan Henriette
Aaron Havolock
Brandon Fanchette
0 comments:
Post a Comment