JESHI
la Polisi nchini, limesema linafanya uchunguzi kubaini baadhi ya vijana
wanaojiunga na vikundi vya kigaidi, vikiwamo IS na Al-Shabaab ili
wawachukulie hatua za kisheria.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Upelelezi wa
Makosa ya Jinai (DCI), Diwani Athuman, alisema wimbi la vijana hao
kujiunga na makundi hayo yanayopigwa vita duniani kote, linatokana na
ushawishi wa baadhi ya watu.
“Tuna
taarifa za kuwapo baadhi ya vijana wa Kitanzania wanaojiunga na vikundi
vya ugaidi… suala hili ni la kiintelijensia zaidi, hatuwezi
kulizungumzia kiundani, tunaendelea kulifanyia kazi, tutakapofikia
sehemu nzuri tutawaambia,” alisema Athuman.
Alisema
wakati suala hilo linaendelea kufanyiwa kazi, jeshi hilo liliendesha
operesheni maalumu ya siku mbili, ambayo ilishirikisha nchi 26 za Afrika
Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Alizitaja
nchi hizo kuwa ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Angola,
Botswana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Lesotho, Malawi,
Madagascar, Mauritius, Msumbuji, Namibia, Afrika Kusini, Swaziland,
Zambia, Zimbabwe, Comoro, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Shelisheli, Sudan
Kusini na Somalia.
Alisema
operesheni hiyo iliyojulikana kama ‘Operesheni Usalama III’
ilishirikisha nchi zaidi ya 26 na ilisaidia kukaguliwa kwa magari 1,632
ambayo kati ya hayo, 10 yalikuwa ya wizi huku matano yalibainika
yameingiliwa ‘chases’.
Alisema
operesheni hiyo pia ilisaidia kukamatwa pikipiki 12 za wizi, huku 18
zikiendelea kufanyiwa uchunguzi zaidi kutokana na kutokuwa na vibali
halali.
Athuman
alisema operesheni hiyo ilisaidia pia kukamatwa aina mbalimbali ya dawa
za kulevya, zikiwamo heroine gramu 83, bangi kilogramu 398.6, mirungi
kilogramu 30, bunduki aina ya shotgun moja, gobole 11, risasi 104, mkuki
mmoja na vipande 15 aina ya exprojel v6, cotex na detonator.
Alisema
walikamata wahamiaji haramu 43 maeneo mbalimbali nchini, kati yao 18
ni raia wa DRC, ambao walikamatwa mikoa ya Rukwa na Kagera, wakati 22
wanatoka Burundi waliokamatwa mikoa ya Shinyanga, Tabora na Kagera na
raia wawili wa Rwanda walikamatwa Kagera na mmoja wa Kenya alikamatwa
Tabora.
“Katika
operesheni hii tulifanya ukaguzi katika kampuni mbalimbali zinazofanya
biashara ya madini ambapo tatu zilionekana kukosa uhalali wa kupewa
leseni ya kuendelea kufanya biashara ya madini,
“Kampuni
hizi ni Delicore Metal Company Ltd, Madandwa Gold Mining Export Import
(T) Ltd na Alex Mining Co. Ltd, na tatizo lao linaendelea kushughulikiwa
na Wizara ya Nishati na Madini. Pia yalikamatwa madini aina ya Acquqmiline Smoky Quartz kilogramu 20.
Alisema
pia walikamata gamba moja la kasa mkoani Ruvuma, mbao 410 zilizokuwa
zikisafirishwa bila kibali mikoa ya Pwani, Iringa na Morogoro, nyama ya
pundamilia kilo 45 na bidhaa bandia.
0 comments:
Post a Comment