TP Mazembe imekubali kipigo cha mabao 3-2 ikiwa ugenini dhidi ya Medeama katika mechi ya Kombe la Shirikisho, leo.
Ushindi
huo wa Medeama, maana yake imefikisha pointi 8 ambazo haziwezi kufikiwa
na Yanga huku Mazembe ikiwa kileleni na pointi 10.
Baada
ya ushindi wa Medeama, maana yake rasmi Yanga ambayo jana iliifunga Mo
Bejaia imeshindwa kufuzu hatua ya nusu fainali licha ya kuwa na mchezo
mkononi.
Yanga
inabaki na pointi nne mkiani, huku Mo Bejaia ikilazimika kutupa karata
yake ya mwisho kwa kutaka kuifunga Medeama katika mechi ya mwisho ili
ifikishe pointi nane huku ikijaribu kuangalia wastani wa mabao ya
kufunga na kufungwa.
Yanga itamaliza mechi yake ya mwisho dhidi ya TP Mazembe ikiwa ugenini mjini Lubumbashi.
Yanga itamaliza mechi yake ya mwisho dhidi ya TP Mazembe ikiwa ugenini mjini Lubumbashi.
0 comments:
Post a Comment