Sunday 4 September 2016

#BURUDANI>>>> Video ya wimbo ‘Waache Waoane’ imekuwa video ya kwanza ya Chege kufikisha views milioni 1 YouTube.

Licha ya Chege Chigunda kufanya nyimbo nyingi kali lakini hakuwa na nyimbo ambayo video yake iliweza kufikisha views milioni 1 YouTube. Lakni video yake mpya ya wimbo ‘Waache Waoane’ aliyomshirikisha Diamond Platnumz imekuwa ni video yake ya kwanza kufikisha views milioni 1 ndani ya wiki 4.

 Video ya wimbo uliyopita ‘Sweety sweety’ ambao alimshirikisha Runtown wa Nigeria na Uhuru wa Afrika Kusini una views 697,242 ndani ya miezi nane toka itoke.

Hii ni dalili nzuri kwa muziki wa Tanzania kwani wasanii wengi wa Afrika Mashariki wameshindwa kufikia hatua hii ambayo wasanii wa Tanzania wanaifikia.

Pia hivi karibuni video ya wimbo ‘Inde’ ya msanii mkongwe wa muziki Dully Skyes iliweza kufikisha views milioni 1 ndani wiki mbali.

0 comments:

Post a Comment