Saturday, 17 September 2016

#BURUDANI>>>>MOROGORO IMOOO!!,KESHO TIGO FIESTA NDANI YA JAMHURI STADIUM.FAHAMU ZAIDI HAPA.

WASANII 18 wa muziki wa Bongofleva watapanda jukwaa moja kwenye tamasha la Tigo Fiesta litakalofanyika kesho kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro.


Wasanii hao watatoa burudani kwenye tamasha hilo linalodhaminiwa na kampuni ya Tigo ambalo linafanyika katika mikoa mbalimbali nchini.
Nyota hao wanaotarajiwa kutoa burudani katika tamasha hilo ni pamoja na Ben Pol, Christian Bella, Jux, Nandi, Mr Blue, Chege,Dully Sykes, Fid Q na Darassa.

Wengine ni Linah, Vanessa Mdee, Mau, Moni,Snura, Man Fongo, Baraka Da Prince, Bonge la Nyau pamoja na kundi la Weusi linaloongozwa Joe Makini.

Tamasha la Tigo Fiesta litafanyika katika mikoa 15 ambapo tayari limefanyika katika mikoa mitano ya Mwanza, Kagera, Shinyanga, Singida na Dodoma.

<<<<DOWNLOAD APPLICTION KWENYE SIMU YAKO HAPA>>>

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment