Sunday 4 September 2016

#BURUDANI>>>Niliwahi kuchukiwa baada ya kuleta muziki wa kuimba – Dully Sykes.Fahamu zaidi hapa.

Dully Sykes amedai kitendo chake cha kubadilisha muziki kutoka kwenye Hip Hop mpaka kwenye kuimba kulifanya baadhi ya wasanii wenzake kumchukia.
Muimbaji huyo ni mmoja kati wa wasanii wachache wapo muda mrefu kwenye tasnia ya muziki ikiwa ni zaidi ya miaka 15 lakini mpaka leo hii anaendelea kufanya vizuri kwa kuachia hit kibao na kuwatoa jasho wasanii walioanza kufanya muziki hivi karibuni.


“Watu wa Hip Hop walinipiga sana vita mpaka ikafikia wakati rafiki zangu wakanichana kidogo wakina mwana FA na Jay Moe,” ameiambia BBC.


Wimbo ambao Dully anadai kuwa alichanwa na wasanii haoni ‘Ingekuwa Vipi’ ambao jina lake limetajwa ndani ya wimbo huo japo siyo peke yake aliyetajwa.


“Ingekuwa vipi Dully Sykes angeimba hardcore mashairi kama Jay Moe neno wanasesere nina imani lisingekuwepo,” Mwana FA anarap kwenye Ingekuwa Vipi.


Kwa sasa msanii huyo anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Inde’ aliomshirikisha Harmonize ambao umefanikiwa kutazamwa kwa zaidi ya milioni 1 na laki 2 ndani ya wiki tatu kwenye mtandao wa YouTube.

0 comments:

Post a Comment