Home »
Michezo
» #MICHEZO>>>BAADA YA RIHANNA, SASA KWA RONALDO AMEBAKI TAYLOR SWIFT TU!..FAHAMU ZAIDI HAPA.
Ronaldo & Rihanna
Nyota
wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo anajulikana na anatajwa kuwa ndiye
mwanamichezo ambaye ana wafuasi wengi katika mitandao ya kijamii lakini
tofauti na hapo katika fani nyingine pia anawafunika akiwa amesaliwa na
mtu mmoja tu.
Mreno huyo ambaye anajulikana kwa kupenda kupendeza
ana jumla ya wafuasi milioni 238 katika kurasa zake kwenye mitandao ya
Facebook, Twitter na Instagram. staa pekee ambaye hajamfikia ni
mwanamuziki Taylor Swift ambaye ana wafuasi milioni 246.
Takwimu hizo ni kwa mujibu wa Taasisi ya Hispania kutoka jinni la Madridi inayojulikana kwa jina la Apple Tree Communications.
Ronaldo
amewazidi mastaa wengi wa fani nyingine wakiwemo Katy Perry, Selena
Gomez na Rihanna ambao wana wafuasi milioni 219, milioni 205 na milioni
190.
Utafiti huo unaonyesha kuwa asilimia kubwa ya wafuasi ni wanawake wenye mri wa kati hasa kutoka Marekani.
Taylor Swift & Ronaldo
Februari,
mwaka huu Ronaldo ndipo alipoanza kusika rekodi ya kuwa mwanamichezo
aliyefikisha wafuasi wengi katika mitandao ya kijamii kwa kusikisha
milioni 200, baada ya hapo amekuwa akiongeza idadi.
Kwa sasa
Ronaldo anawazidi wanamichezo wengine mastaa akiwemo mpinzani wake
kutoka Barcelona, Lionel Messi na wachezaji nyota wa kikapu, LeBron
James, Michael Jordan, Kobe Bryant, Kevin Durant na Steph Curry.
Related Posts:
#MICHEZO>>>>FIFA YAILIMA FAINI SIMBA, YAPANGA KUISHUSHA DARAJA.Fahamu zaidi hapa.
SHIRIKISHO la Soka la
Kimataifa (FIFA), limeipiga faini ya Franc 2,000 za Uswisi (Sh
4,582,000), Klabu ya Simba baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kupuuza
maagizo ya Idara ya Utatuzi wa Migogoro (Desputes Resolution Cha… Read More
#MICHEZO>>>>HUYU NDO MCHEZAJI MWINGINE WA CAMEROON ALIYEFIA UWANJANI JANA.Fahamu zaidi hapa.
Kama ni mfuatiliaji mzuri wa mitandao ya soka barani Ulaya huenda utakuwa umekutana na taarifa za kusikitisha kwa taifa la Cameroon, usiku wa May 6 2016 Cameroon na Afrika kwa ujumla ilipata taarifa za kushtusha, baad… Read More
#MICHEZO>>>>STEWART HALL KUIPA AZAM MKONO WA KWAHERI.Fahamu zaidi hapa.
Siku moja baada ya TFF kuipoka Azam FC pointi tatu kutokana na
kumtumia Erasto Nyoni aliyekuwa anakadi tatu za njano kwenye mchezo wao
dhidi ya Mbeya City, kocha mkuu wa Azam FC Stewart Hall amefikia uamuzi
wa kuachana n… Read More
#MICHEZO>>>AZAM WAKUBALI YAISHE, KUKOMAA NA KOMBE LA FA.Fahamu zaidi hapa.
SIKU moja baada ya
Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) kuipokonya pointi tatu timu ya
Azam kwa kosa la kumchezesha beki wao Erasto Nyoni aliyekuwa na kadi
tatu za njano, Uongozi wa timu hiyo umelijia juu shir… Read More
#MICHEZO>>>>STAR WA MANCHESTER UNITED AMEKIMBILIA KWENYE MOVIE.Fahamu zaidi hapa.
Midfielder wa Manchester United Bastian Schweinsteiger anajiandaa kucheza tangazo jipya la iPhone app, Clash of Kings.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani akiwa na kikosi cha Old
Trafford ndani ya msimu wake wa … Read More
0 comments:
Post a Comment