Goli pekee la kika ya 76 la mshambuliaji wa Manchester City Kelechi
Iheanacho limeendeleza rekodi ya Stars kushindwa kupata ushindi mbele ya
Nigeria ambapo kwa mujibu wa rekodi, Stars haijafanikiwa kupata ushindi
ushindi mbele ya The Super Eagles tangu timu hizo zilipoanza kukutana.
Stars ilisafiri hadi Nigeria kwenda kucheza mchezo wa kukamilisha
ratiba katika Kundi G ikiwa ni mechi ya kutafuta nafasi ya kufuzu
kucheza fainali za michuano ya mataifa ya Afrika (AFCON 2017) nchini
Gabon.
Hadi hatua ya makundi inamalizika, Stars haijafanikiwa kupata ushindi
katika Kundi G baada ya Chad kujitoa kwenye kundi hilo kutokana na
matatizo ya kifedha. Ushindi pekee wa Tanzania ulikuwa ni dhidi ya Chad
ambapo Stars ilipata ushindi wa goli 1-0 ugenini lakini ushindi huo
ulifutwa baada ya Chad kujiengua.
0 comments:
Post a Comment