Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wafanyakazi na watendaji wa kiwanda hicho baada ya kutembelea kiwanda kwa mara ya kwanza tangu ashike wadhifa huo kwa lengo la kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa kiwandani hapo akiwa katika ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani Mtwara.
Amesema
kiwanda cha kuchakata gesi asilia ni hazina kubwa kwa Taifa hivyo ni
kikalindwa na kutunzwa ipasavyo kutokana na umuhimu wake katika
uzalishaji wa nishati ya umeme kwa maendeleo ya nchi.
Makamu
wa Rais pia amewashukuru na kuwapongeza wafanyakazi wa kiwanda hicho
cha kuchakata gesi asilia cha Madimba na amewahakikishia kuwa serikali
itaendelea kuwajali na kuwathamini katika utendaji wao wa kazi na kwamba
serikali itahakikisha wafanyakazi wa kiwanda hicho wanapewa motisha ya
kutosha ili waongeze maradufu utendaji wao wa kazi ili malengo ya
serikali ya kuleta maendeleo kwa wananchi kupitia viwanda inatimia kwa
sababu taifa litakuwa na nishati ya umeme ya uhakika.
Makamu
wa Rais amewataka watendaji wa Shirika la Maendeleo la Petroli (TPDC)
ambalo linasimamia mradi huo kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya
kusaidia huduma za jamii katika vijiji vinavyozunguka mradi huo kila
mwaka ili wananchi waweze kuwa walinzi wa mitambo hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba Mhandisi Leonce namna gesi inavyopokelewa na kuchakatwa na kusafirishwa kwa watumiaji.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akiangalia mfumo wa uendeshaji na usalama wa kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba mkoani Mtwara.
0 comments:
Post a Comment