Shirikisho
la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini limemuomba Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi wa hesabu za Sh
bilioni 1.74 za ada ya uombaji mikopo kwa mwaka huu katika Bodi ya
Mikopo (HESLB) ili kujua matumizi ya fedha hizo kwa kuwa kuna mapungufu.
Aidha,
shirikisho hilo limedai kubaini hujuma katika bodi hiyo zinazofanywa
kwa makusudi ili kuchafua utendaji wa serikali iliyopo madarakani.
Hayo
yalisemwa jana na Katibu Mtendaji wa shirikisho hilo, Daniel Zenda
alipokuwa anazungumzia tuhuma za hujuma hizo, akidai zinafanywa kwa
makusudi ili kurudisha nyuma jitihada njema za serikali.
Alisema
ofisi ya CAG inapaswa kufanya ukaguzi wa Sh bilioni 1.74 fedha ambazo
zilitokana na ada ya uombaji wa mikopo kwa mwaka huu ambapo kila
mwanafunzi alitoa Sh 30,000 kwa waombaji 54,000.
Alisema
ni muhimu kujua matumizi ya fedha hizo kutokana na upungufu
uliojitokeza katika upitiaji wa sifa na vigezo vya wanaostahili kupata
mkopo.
Alifafanua
kuwa wanatambua hatua ya serikali katika kuhakikisha wanafunzi wenye
sifa wanapata mikopo kwa wakati ambapo takribani Sh bilioni 80
zimeongezwa kwenye bajeti ya bodi hiyo ili kuwezesha mikopo kwa
wanafunzi wote wenye sifa.
Zenda
alisema Sh bilioni 487 zimepitishwa katika bajeti ya mwaka huu na mwaka
jana ilikuwa chini ya makadirio ya Sh bilioni 350, lakini pamoja na
kuongezeka kwa fedha hizo idadi ya wanafunzi walionufaika na mikopo
imekuwa pungufu.
“Mwaka
uliopita wanufaika wa mikopo walikuwa 53,000 na mwaka huu wanufaika
wanafunzi 25,700 pamoja na ongezeko la makadirio ya zaidi ya Sh bilioni
137 kwenye bajeti ya Mikopo bado wanafunzi wengi hawajafikiwa,” alisema.
0 comments:
Post a Comment