MATUKIO yanayohusiana na mapenzi yameendelea kuwa tishio nchini baada ya
mwanamke mmoja, Helen John (25) kumwagiwa tindikali na mpenzi wake na
kumfanya jicho lake lisione.
Hellen ambaye ni mkazi wa kijiji cha Kwamhosi kata ya Nkumba wilayani
Muheza mkoani Tanga, alipata mkasa huo Aprili 17, mwaka huu.
Akizungumza na Nipashe , alisema chanzo cha tukio hilo ni baada ya
kukosana na mpenzi wake huyo na kufanya kuishi tofauti bila mawasiliano
hadi siku ya tukio ingawa walikuwa wamezaa mtoto mmoja.
Hellen alisema siku ya tukio kijana huyo aliyemtaja kwa jina la Ally
Khamis alikwenda nyumbani kwao kwa lengo la kumbembeleza kurudiana
lakini alikataa kwa madai kuwa hataki kuishi na mwanaume huyo kutokana
na vitendo vya ukatili ambavyo amekuwa akimfanyia.
Alisema baada ya kukataliwa kijana huo usiku alikwenda kumuwmwagia
tindikali machoni na kisha kukimbia lakini ulifanyika msako kwa
wanakijiji na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa na kupelekwa katika kituo
cha polisi Muheza.
Credit - Nipashe
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment