Shirika la umeme Tanzania TANESCO limesema kuwa utunzaji wa vyanzo vya
maji vya mto ruaha mkuu ambavyo vinapatikana wilaya za Wanging’ombe na
Makete mkoani Njombe unasaidia kuongeza Maji yanayohitajika katika
ufuaji wa umeme kwenye mabwawa ya Mtera na Kidatu.
Kaimu mkurugenzio mtendaji wa TANESCO Dr Tito Mwinuka akiwa katika
ziara ya kikosi kazi maalumu kilicho undwa Hivi karibuni na makamu wa
raisi Samia Suluhu Hassani akiwa mkoani Iringa kwaajili ya kutunza
ikolojia ya mto Ruaha mkuu amesema kuwa Asilimia 41 ya umeme
unaozalishwa hapa nchini unategemea maji na huwa ni bei nafuu.
Mwenyekiti wa kikosi hicho kilichopangiawa kuzulu vyanzo vya maji vya
mto Ruaha mkuu katika mkoa wa Njombe Katibu Tawala wa mkoa wa Njombe
Jackson Ole Saitabau amesema lengo la kikosi hicho kuundwa ni kurudisha
hali ya utiririshaji wa maji katika mto ruaha mkuu.
Baadhi ya wananchi wilayani Wangingombe wanaotunza vyanzo mto Ruaha mkuu
vya Mbukwa na Mtitafu vilivyoko katika vijiji vya Nyumbanitu, Igima na
Mlevela wameeleza changamoto zinazowakabili katika kuhifandhi vyanzo
hivyo pamoja na kutoa mapendekezo kwa serikali kusimamia sheria.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment