Mbunge
wa Arusha Mjini, Godbless Lema amewaonya watu aliodai kuwa wamemuweka
kwenye orodha ya wabunge kumi na moja wanaotakiwa kutekwa.
Akizungumza
leo na waandishi wa habari mjini Dodoma, Lema amedai kuwa yeye haogopi
vitisho vya kutekwa na kwamba wanaopanga kumteka wanapaswa kufahamu kuwa
hawatafanikiwa na kwamba hakuna atakayeweza kusababisha kifo chake
isipokuwa Mungu pekee.
“Ninawaonya
watekaji, kwamba ninamjua Mungu ninaemwamini, kwamba hawataliona kaburi
langu wala mauti yangu kwa sababu Mungu ninayemuamini najua nguvu zake
na najua uwezo wake,” alisema Lema.
“Kwahiyo mimi kutekwa haitawezekana, kuuawa na mtu haitawezekana kwa sababu namtumaini Mungu kwa nguvu zangu zote,” aliongeza Mbunge huyo.
Kauli
hiyo ya Lema imekuja kufuatia kauli ya Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein
Bashe aliyeeleza jana Bungeni kuwa alionywa na baadhi wa watu wakiwemo
mawaziri kuwa yeye ni miongoni mwa wabunge kumi na moja walio kwenye
mpango wa kutekwa na genge la watu wasiojulikana.
==>Msikilize hapo chini akiongea
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment