Baada ya kamati tendaji ya Yanga kupitia kwa mjumbe wake Salum Mkemi
kutanganza kupinga malalamiko ya Simba dhidi ya Kagera Sugar kwa
kumtumia mchezaji wao Mohamed Fakih kwenye mechi kati ya Kagera Sugar
dhidi ya Simba, afisa habari wa Simba Haji Manara ametoa taarifa rasmi
akiwataka Yanga kutulia.
Kuna taarifa iliyotolewa na klabu ya Yanga inayoonyesha kuishinikiza
Bodi ya ligi kutokutenda haki juu ya rufani yetu dhidi ya klabu ya
Kagera Sugar kwa kumchezesha mchezaji Mohammed Fakih aliyecheza dhidi
yetu akiwa na kadi tatu za njano ambalo ni kosa kisheria.
Taarifa hiyo ya Yanga iliomnukuu Mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu
hiyo Salum Mkemi aliyeoongea mbele ya waandishi huku akiwa na katibu
mkuu wa klabu hiyo Charles Boniface Mkwasa iliitaka bodi kutokutoa
points kwa Simba eti kwa kuwa hizo points zitawaathiri Yanga kwenye
kutetea ubingwa wao ambao kwa sasa upo rehani, pia taarifa hiyo
imeonyesha Yanga wanao ushahidi kuwa Fakih ana kadi mbili za njano.
Klabu ya Simba inawaambia viongozi wa Yanga wanayo mambo ya msingi ya
kuwashughulisha, ikiwepo kutafuta mishahara ya wachezaji wao iliokwama
kwa miezi kadhaa kama inavyoripotiwa mitandaoni na kwenye vyombo vya
habari,pia waangalie namna bora ya kuurejeshea hadhi uwanja wake wa
mazoezi wa Kaunda ili upate kuchezeka tena na sio ulivyo hivi
sasa,ambapo umegeuka kama bwawa la kufugia kambale,,ni kushangazwa
kulikochupa mpaka kufuatilia rufani isiyowahusu,Hii ni rufani ya Simba
dhidi ya Kagera sio wao Yanga.
Tunaamini bodi haitafanya maamuzi kwa shinikizo la yoyote yule,na
hatutarajii kuona porojo walizozisema leo zitaondoa ukweli uliopo mezani
kwao ambao klabu yetu imeuwasilisha
Mwisho niwaombe washabiki wetu watulie na waiachie bodi ifanye maamuzi yake ambayo tunaamini yatatoa haki kwa anayestahili.
IMETOLEWA NA.. Haji S Manara
Mkuu wa Habari wa Simba Sc
SIMBA NGUVU MOJA
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment