Mbunge
wa Nkasi Kaskazini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ali Mohamed
Keissy amefunguka na kusema wasanii ambao wanaandika nyimbo za
kumtukana na kumkashfu Rais Magufuli wanapaswa kupata kibano zaidi ili
waache tabia hiyo
Mbunge
huyo amesema hayo leo bungeni na kusema angeaachiwa yeye dakika mbili
tu wangeona ni nini angewafanya, hivyo kuendelea kuwatetea wasanii hao
ni jambo ambalo si sawa, na kusema wasanii hao wajaribu kwenda Rwanda au
nchi za kiarabu waone jinsi watakavyonyongwa.
"Mtu anaimba wimbo wa matusi kumtukana Rais mwanzo mpaka mwisho halafu anaachiwa nchi gani hii? Utawala gani huu? Wewe mtu unamtukana Rais unaachiwa?,
aende Rwanda kule au nchi za kiarabu watakunyonga. Unamtukana Rais wa
nchi wewe umekuwa nani? Uhuru gani huu, Demokrasi gani hii? Unaimba wewe
nyimbo na mtu wa studio anarekodi ama kweli huu si utawala wangeniachia
mimi dakika mbili ili niwaoneshe hawa" alisema Mbunge Kessy
Keissy anasema ni jambo ambalo haliwezekani mtu kumuimba Rais anamtukana na wewe kuendelea kushabikia huku akidai kuwa yeye ameusikiliza wimbo wa Roma na kusikitishwa na kile kilichoimbwa.
"Ukiusikia
huo wimbo wa Roma Mkatoliki ndugu zangu ni wimbo wa aibu sana,
haiwezekani mtu na akili yako unasikia wimbo kama ule halafu
unashabikia mtu, haiwezekani kusema kweli ni makosa, ni kukosa adabu
Rais wa nchi hatukanwi popote pale haiwezekani nendeni nchi zingine,
nenda Rwanda hapo nenda Burundi nenda DRC Congo ukaangalie
watakushugulikia, nyinyi mnacheka cheka hapa. Rais haiwezekani kumchezea
namna hii huu ni utovu wa nidhamu" alisisitiza All Keissy
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment