WAKATI msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’,
akiendelea kusaka faraja ya moyo kutokana na kudai kuwa amekuwa
akikabiliana na vitisho, mama yake mzazi ameamua kuondoka nyumbani
kwake akihofia kuuawa.
Nay aliingia kwenye mgogoro na serikali kutokana na wimbo wake wa
Wapo uliosababisha ashikiliwe na jeshi la polisi pamoja na wimbo huo
kufungiwa na Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) lakini aliokolewa na
kwa amri ya Rais John Magufuli.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Nay amesema pamoja na tamko la
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe,
kutoka kwa rais, kuruhusu wimbo wake uchezwe kote, ameendelea kuwa na
vitisho kila kukicha kutoka kwa watu asiowafamu.
“Ninaishi kwa mashaka makubwa, tangu nilipoachia wimbo huu, maana
kumekuwa na mfululizo wa kupigiwa simu na meseji za watu wakinitishia
maisha jambo ambalo limepelekea hadi mama yangu kuamua kuhama nyumbani
kwangu na kurudi kwake.
“Kabla sijatoa wimbo huu nilikuwa naishi na mama nyumbani kwangu,
lakini ameamua kuondoka kufuatia kutishiwa maisha kila kukicha, lakini
baya zaidi vitisho hivyo vimenifanya mimi na mama kupishana mawazo
ambapo ameniambia niachane na wimbo huo, tena ikiwezekana niachane na
muziki ili nifanye biashara zingine jambo ambalo sijamkubalia.
“Nafikiri kutomkubalia kwangu dhahiri nahisi itakuwa ndicho kisa
cha kuamua kuondoka na kurudi nyumbani kwake, napata tabu sana na wimbo
huu, lakini naamini mimi ni mtu wa misimamao hivyo siwezi kuachana na
muziki kisa vitisho.
“Katika maisha hakuna jambo rahisi hasa kama wewe ni mpambanaji,
vitisho kama hivi sitaki kuvipatia nafasi ya kuniharibia maisha kwani
mimi ninachokifanya ni kuwakilisha mawazo ya wazalendo wengi ambao
imekuwa ni ngumu kila mmoja kufikisha maoni yake kwa jamii.
“Kuna watu wanadhani nilipoitwa na Mwakyembe nilienda kushikiwa
akili ili nibadili muziki wangu lakini ukweli ni kwamba, kule alikuwa
akinipa ushauri wa kawaida tu, hivyo hakuna jambo ambalo
amenibadilisha kwenye muziki wangu na nitaendelea kupigania
ninachokiamini ili nitimize ndoto yangu.
“Kifo kipo tu lakini wengi t u m e k u w a waoga wa kutangulia
hasa ukifikilia jamii inayokuzunguka, Wapo imenikutanisha na watu
nisiowafahamu, maana nakumbuka siku mbili nyuma zilizopita nilipigiwa
simu na mtu nisiyemjua akidai anahitaji kufanya biashara na mimi hivyo
nikaenda kuonana nae Ubungo.
“Huwezi kuamini ningekua muoga basi nisingemsikiliza maana baada ya
kukutana alinitoa chemba na kuanza kunihusia juu ya kuachana na wimbo
huo akidai watu wamejifanya kunichunia lakini hakuna anayefurahishwa,
hivyo kama nataka amani iendelee basi niuache na kingine akaniamia niwe
makini kwani kuna watu wana nia mbaya na mimi.
“Kusema kweli nimeshatishwa sana lakini watu wanachotakiwa kujua
kama kifo kipo basi nitakufa kwa kuwatetea mamilioni ya mashabiki zangu,
ila suala la kushikiwa akili au kubadilishwa gia yangu hapa halina
nafasi,” anasema Nay.
Ikumbukwe kwamba mwishoni mwa wiki iliyopita Nay baada ya kutoka
Dodoma, alikoenda kuitikia wito wa waziri Mwakyembe, alisema
amefarijika kwa namna moja au nyingine hasa baada ya kukutana, kwani
walipata muda wa kuketi na kuzungumza mambo mengi juu ya sanaa ya
muziki.
Huku akimtaka kuwa makini na tunzi zake kwani zimekuwa na mfululizo
wa maneno ya kuwagusa watu moja kwa moja hivyo awe makini kwani kuna
wengine huwa si wavumilivu kwani asipojiahadhali wanaweza kuja kumdhuru
kwa namna moja au nyingine.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment