IKIWA katika hali ya kuyumba kiuchumi na kushindwa kuwalipa
wachezaji wao mishahara kwa wakati, neema imeanza kuwaangukia baada ya
kampuni ya SportsPesa ya Kenya kutaka kuwamwagia fedha iwapo mkataba wao
utafanikiwa.
Yanga itakuwa ni ya tatu kwa timu za Afrika Mashariki kuingia
mkataba wa fedha nyingi iwapo watakapofanikiwa kumalizana kumalizana na
Kampuni ya SportsPesa ya Kenya.
Iwapo mkataba huo utafanikiwa, Yanga na kampuni hiyo ya SportsPesa
watasaini mkataba wenye thamani ya bilion 4.5 ambapo utakuwa ni wa
miaka mitano ambapo kwa mwaka utakuwa na thamani ya Sh milioni 900.
Uongozi wa Yanga leo unatarajiwa kutakutana na wawakilishi wa
kampuni hiyo, ambapo wakikubaliana wataingia mkataba huo wa miaka mitano
ambao kila mwaka utakuwa na nyongeza ya asilimia sita ya fedha.
Awali, SportsPesa walileta mapendekezo katika klabu ya Yanga
kuhusiana na mkataba huo lakini ulikatiliwa kutokana na mkataba huo
kutokukidhi vigezo nan kuwa na maslahi na wakawapelekea mapendekezo yao
na namna gani wanataka mkataba huo uweje.
"\Leo wawakilishi wa SportPesa watakutana na uongozi wa Yanga ili
kumalizana nao juu ya mkataba wanaotaka kuingia na hiyo ni kutokana na
kufika makubaliano ya kimkataba," kiisema chanzo kutoka kamati ya
utendaji ndani ya klabu hiyo.
Alipotafutwa Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa, ambaye alisema wapo kwenye hatua za mwisho za kuingia mkataba na SportsPesa.
"Napenda nizungumze kitu kilichokua tayari au kimekamilika hatua
ya kuingia mkataba na SportsPesa bado, ila tutakutana nao kwa mazungumzo
ya mwisho ambayo yatatoa jibu kama watatudhamini au la.
"Tunazungumza na SportsPesa kwa kuwa hawa wamekuja moja kwa moja
kwetu tofauti na kampuni nyingine ambazo zinataka kutudhamini, lakini
ipo kampuni tuliyoipa jukumu la kufanya mazungumzo nao nasi kutuletea
taarifa ya kila kinachoendelea." alisema Mkwasa.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment