Saturday 25 July 2015

SAFARI YA MATUMAINI PART II YAZIDI KUWAUMIZA VICHWA CCM.




*SAFARI YA MATUMAINI PART II YAZIDI KUWAUMIZA VICHWA CCM, Katika hali isiyokuwa ya kawaida taarifa ambazo zimekuwa zikisambaa katika mitandao ya kijamii zihusuzo Jemedari EDDO kuhitajiwa na Watanzania kuwaondolea umasikini nje ya Chama chake cha CCM ambacho amekulia kwa muda mwingi wa maisha yake ni kwamba CCM wanahaha juu ya Mustakabali wa uhai wa chama hicho. Taarifa zinazidi kuthibitika kuwa sasa ni wazi kuwa *Safari ya Matumaini sehemu ya pili imewadia na MAFURIKO yameendelea kuwakumba hususani Viongozi wakubwa wa CCM ambao wamekuwa wakijitahidi kumsihi Mpambanaji huyo kubaki CCM bila mafanikio.
“Mwenyekiti amekuwa akimpigia simu mzee mara nyingi sana lakini mzee amekuwa kimya" "Unajua Mwenyekiti alifikiri kama mzee hawezi kuondoka na akafikiri kuwa yale mafuriko ni utani utani kumbe ni ya kweli, na alidhani ni mchezo tu, sasa hivi kichwa kinamuuma sana", Kilisema chanzo cha habari cha kuaminika. Inasemekana Mh. kati ya siku chache zijazo anaweza rasmi kutua UKAWA,
Haya yamekuwa yakionekana kutoka kwa viongozi ambao wanaunda UKAWA kwa kuanza kuwa wazi, Vijana wanasema "wanafunguka" Zitto Kabwe nae ameshughudiwa akifunguka kwa kusema "Wiki ya kuanzia Jumatatu tarehe 27 Julai 2015 itashuhudia mabadiliko makubwa sana kwenye siasa za Tanzania., Kuimarika kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa ni jambo jema kwa Nchi yetu". Lakini hata Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema amekaririwa na Gazeti la MTANZANIA akisema "Tutampokea Kigogo mkubwa wa ccm na wenyeviti wa mikoa na wilaya dar es salaam.
 Nchi itatikisika" Taarifa za kuaminika zinasema hata Mgombea Urais wa CCM Mh. Magufuli amekuwa sio deal tena bali LOWASSA ndiye amekuwa gumzo hasa kwa Viongozi wa Chama hususani Mwenyekiti akihaha juu ya kuzuia Mafuriko lakini inashindikana na wananchi wanasema wanajipanga kumshawishi LOWASSA ahamie UKAWA.

0 comments:

Post a Comment