Tuesday 28 July 2015

#YALIYOJIRI>>Lowassa atangaza kujiunga rasmi na CHADEMA, apokea mwaliko wa UKAWA ajing'atua CCM akabidhiwa kadi ya CHADEMA.


Hatimaye aliyekuwa mbunge wa Monduli kwa tiketi ya CCM Edward Lowassa amejiunga rasmi na chama cha demokrasia na maendeleo Chadema huku akisisitiza kuwa hakuusiki kwa namna yoyote ile na sakata la Richimond.
Mwaka 1995 akihutubia mkutano mkuu wa CCM mjini Dodoma, baba wa taifa alisema miaka 25 baada ye moja ya vigogo wa CCM anakiri kwa kusema mabadiliko ya kweli yako ndani ya upinzani.

Bw Edward ametoa kauli hiyo ambayo inavunja ukimya na minongono ya muda mrefu baada ya kukatwa katika harakati za kuwania nafasi ya urais ndani ya CCM, anasema alichokishuhudia Dodoma ni ubakaji wa demokrasia.

Toka mwaka 2008 alipojiuzulu nafasi ya uawziri mkuu jinamizi la sakata la Richimond limekuwa likimuandama, anasema sasa inatosha.

Mwenyekiti wa Chadema akizungumza mara baada ya kuwakabidhi kadi za uanachama Edward na mke wake Bi Regina Lowasa anasema chama chake kimefanya maamuzi sahihi kumualika Bw Edward Lowasa.

Hafla hiyo ya kumkabidhi Lowasa kadi ya Chadema imefanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuliwa na familia yake ikiwa ni pamoja na viongozi mbalimbali wa Ukawa.

UNAKUMBUKA MWAKA-2008
kama kweli wewe mchambuz namfuatiliaji wa siasa ..... kumbuka hiki.............. Lowassa Ngoyai Edward 2008 . "Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru sana kwa kunifanya msemaji wa kwanza katika hoja hii. Lakini la pili, nimpongeze Dk. Harrison Mkwakyembe, Mwenyekiti wa kamati Teule kwa kuwasilisha kwa mbwembwe nyingi sana taarifa yake, mbwembwe zilikuwa nzuri kweli. Kwa kazi nzuri kwa maoni yao, wamewasilisha vizuri. Lakini nimesimama kuweka kwenye kumbukumbu kutoridhika kwangu na jinsi kazi hiyo ilivyofanywa. Mheshimiwa Dk. Mwakyembe ni Mwanasheria, tena Daktari alikuwa anafundisha Chuo Kikuu. Moja ya vitu alivyokuwa anafundisha ni "Natural Justice". Mheshimiwa Spika, wewe ni Mwanasheria unafahamu suala la Natural Justice. Kwamba Kamati Teule imesikiliza watu wengine wote pamoja na wanaoita minong'ono ya mitaani, wamesafiri mpaka Marekani kutafuta mashahidi, lakini mimi ambaye ni mmoja kati ya watuhumiwa mle hawakunihoji hata siku moja. Mheshimiwa Spika, nimesimama kueleza masikitiko yangu. Ofisi ya Bunge mpaka ofisini kwangu hata kama wangeniita ningekwenda kwa miguu kama hamna gari na nilikuwa tayari kufanya hivyo. Hawa ni watu makini sana siwezi kuamini kwamba wanaweza wakafanya oversite kama hiyo. Kwa sababu katika kila hoja walizojenga wamesema Waziri Mkuu ilikuwa hivi. Kulikuwa na shida gani kuja kuniuliza Waziri Mkuu wanasema uliotoa dokezo hili ni sawa sawa kweli? Kulikuwa na shida gani kwa mfano kufuata utaratibu wa Westminster kuthibitisha hapo unaposema mwenye Richmond ni fulani uka-lay on the table records na ushahidi kuwa ni fulani. Mheshimiwa Spika, Taifa letu ni Taifa changa, lakini chombo hiki ndiyo mahali pa demokrasia pakubwa katika nchi pote, hapa ndipo penyewe. Kama katika chombo hiki haki haitaonekana kutendeka nchi yetu haitakwenda vizuri. Hapa ndipo tunategemea tuwaonyeshe umakini wetu, umahiri wetu katika mambo ya demokrasia. Kwa nhiyo nilichofanyiwa napenda kuweka kumbukumbu sawa kwamba naona si sahihi, nimefadhaika sana, nimedhalilishwa sana, nimeonewa sana katika hili. Maana zimechukuliwa tuhuma zikaelezwa hapa kwamba hivi ndivyo ilivyo. Mimi sijauliza. Kulikuwa na shida gani kuniuliza, kwa nini muamini minong'ono ya mitaani kuliko maelezo yangu. Sisi wote hapa ni wanasiasa tukianza kuamini minong'ono ya mitaani niambieni mwanasiasa atakayesimama. Hatuwezi, Tume imepewa muda wa kutosha lakini inashindwa kumuona mtu ambaye wanamtuhumu na wanamsema kwa kirefu sana. Mheshimiwa Spika, lakini hata pale uliponinong'oneza ukaniambia una ushahidi wowote? Nilikupa ushahidi huo wa maandishi. Katika taarifa yao hakuna hata moja ya ushahidi ambao umetoka Waziri Mkuu. Kile kitabu cha majedwali kimejaa majedwali mengi pamoja na magazeti mpaka ya Udaku lakini maelezo ya Waziri Mkuu hakuna hata moja. Mheshimiwa Spika, naamini ingekuwa ni heshima wangeiweka halafu wakasema tunakataa kitambulisho hiki kwa sababu hii na hii, hiyo ndiyo imejengwa hoja. Lakini kujenga hoja na kuja hapa Bungeni tunahutubia nchi nzima na kusema Waziri Mkuu amefanya hiki, amefanya hiki bila ya kumsikiliza nachelea kuuliza hivi mtu wa chini itakuwaje? Mheshimiwa Spika, lakini nimetafakari kwa makini sana jambo hili nikajiuliza hivi kulikoni mpaka watu wazima wenye uwezo wao, watu maarufu wenye heshima zao, mpaka wafike mahali waache jambo la msingi kama hilo kulikoni? Mimi nadhani there is a wish which I am going to grant, ni Uwaziri Mkuu. Nadhani tatizo ni Uwaziri Mkuu. Kwamba ionekane Waziri Mkuu ndio amefanya haya, tumuondolee heshima au tumwajibishe. Mheshimiwa Spika, nimetafakari kwa niaba ya chama changu, kwa niaba ya Serikali yangu nimeamua kumwandikia Rais barua ya kumwomba niachie ngazi. Nafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa ili kuonyesha dhana ya uwajibikaji lakini kutokubaliana na utaratibu uliotumika kusema uongo ndani ya Bunge wa kumsingizia mtu. Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii kumshukuru sana Rais kwa heshima aliyonipa ya kutumikia nchi hii kwa Uwaziri Mkuu kwa miaka miwili. Namshukuru sana Mheshimiwa Rais. Nakushukuru wewe, nawashukuru Mawaziri na Manaibu Waziri, nawshukuru Waheshimiwa Wabunge na wanachama wa CCM tuliyosimamia Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi. Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo nashukuru". [07:56, 7/28/2015] rexus regregum: Kwa nini lowasa aliitwa fisadi, hii ni kwa sababu yeye kama waziri mkuu, msimamizi mkuu wa serikali alitakiwa akemee inshu zote za richmond, lakini, yeye alipata shinikizo kutoka kwa Mkulu. Ndiyo maana Kuepuka Mkulu asianguke ilibidi Lowasa ajiuzuru. Vinginevyo Mkulu angetawala Miaka mitatu tu, Na serikari yake ingehanguka. Sasa leo Loawasa ataongea Ukweli kuhusu Richmond,ataongea Vitu vyote ambavyo Mwakyembe aliviacha Kuongea katika Riport yake ,Kwa kuilinda Ikulu.Hata Ongea hayo tu, Pia ataongea kuhusu wamiliki Halisi wa IPTL, pia atagusia Mambo ya Escrow ni nani aliyeengeer Mchakato wote wa Escrow, Ataelezea ni nani Anamiliki Kampuni ya Simba Trust, iliyochukua Bilion 75 kwenye Kashifa

0 comments:

Post a Comment