Sunday 19 July 2015

#YALIYOJIRI>>Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, ametaka kuundwe serikali kamili ya Ukanda wa Ulaya.




Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, ametaka kuundwe serikali kamili ya Ukanda wa Ulaya, itakayokuwa na bunge lake na bajeti yake nzima. Katika mahojiano na gazeti moja la nchini Ufaransa, bwana Hollande amesema kuwa mkasa ulioikumba Ugiriki ni ishara tosha kuwa na ushirikiano wa karibu zaidi kati ya nchi wanachama wa Ulaya na hata utumiaji wa sarafu moja.
Huku hayo yakitokea, nchini Ujerumani, Chansela Angela Merkel ameambia vyombo vya habari kuwa yuko tayari kujadili uwezekano wa kusamehe sehemu ya deni la Ugiriki, lakini kwa sharti kuwa maelezo yote yakamilishwe katika makubaliano ya punde zaidi ya kuukomboa uchumi wake kupitia deni lipya.
Hatma ya Mabenki
Hii leo mabenki ya Ugiriki yanatarajiwa kufunguliwa baada ya kufungwa kwa wiki 3.
Mabenki hayo hata hivyo yanafunguliwa huku kkodi inayotozwa kwa bidhaa muhimu ikipandishwa ikiwemo pia kwa mahoteli na sekta nzima ya usafiri. hatua hii inanuiwa kurejesha imani a raia wa ndani ya Ugiriki na hata jamii ya kimataifa nje ya Ugiriki kufuatia msaada uliokuja kwa masharti ya kufanywa mageuzi kusainiwa wiki iliyopita na hivyo kukomboa nchi hiyo isifilisike.
Bado idadi ya juu zaidi ambayo raia wataruhusiwa kutoa kwenye akaunti zai itaendelea kudhibitiwa na benki kuu ya nchi. awali idadi hiyo iliwekwa kuwa Euro 60 kwa siku, japo sasa kuna matumaini idadi hiyo ikaongezwa hadi Euro 240 kwa siku. hata hivyo wengi wa raia wanasema kuwa kwa muda mrefu uchumi wa nchi hiyo umeharibika na wameshazoea kuishi kwa hata chini ya idadi hiyo kwa siku
Chanzo 
               BBC Swahili

0 comments:

Post a Comment