Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amefanya mabadiliko makubwa kwenye Kamati ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, akiwabadilisha wabunge ishirini na wanne waliokuwa wanaunda kamati hiyo.
Kwa
 mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari, Elimu na 
Mawasiliano cha Ofisi ya Bunge, Ndugai ameteua wajumbe wapya kumi na 
sita wa kamati hiyo ambao pia watakuwa wajumbe wa kamati nyingine.
Taarifa
 hiyo imeeleza kuwa Spika ametumia Mamlaka aliyonayo kikatiba kuunda 
Kamati za Bunge kadri anavyoona inafaa, na kwamba mabadiliko haya 
yamelenga katika kuboresha utekelezaji wa majukumu ya kibunge.
“Kanuni
 ya 116 (3) –(5) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari 2016 
inampa Spika mamlaka ya kuteua wajumbe ili wawe wajumbe katika kamati 
mbalimbali za Bunge ikiwa ni pamoja na mamlaka ya kuongeza, kubadilisha 
au hata kupunguza idadi ya wabunge katika kamati za kudumu za Bunge,” imeeleza taarifa hiyo.
Mabadiliko
 hayo yameanza mara moja kuanzia mwezi huu wa Oktoba na kwamba wajumbe 
wote wameshatumiwa barua tayari kwa maandalizi ya kukutana na kuwachagua
 viongozi wa kamati hiyo.














0 comments:
Post a Comment