Mshindi wa shindano la Big Brother Africa 2014, Hotshots Idris
Sultan, amevunja ukimya na kuzungumzia tetesi ambazo zilikuwa zinazagaa
kwenye mitandao ya kijamii kwamba kuna mtu alimpatia pesa zake kwa ajili
ya biashara lakini akazitumia vibaya kinyume na makubaliano.
Ikumbukwe mshindi huyo wa Big Brother Africa 2014, alipata zaidi ya
milioni 500. Pesa ambayo alidai aliitumia kuwekeza katika biashara
mbalimbali, na baadae aliweka wazi kwamba pesa hizo zilishaisha.
Akizungumza na Bongo5 Ijumaa hii, Idris amesema ni kweli kuna mtu alikuwa anafanye naye biashara lakini akamwingiza mkenge.
“Kuna watu ambao nimeweza kufanya nao kazi, lakini wakaaribu baadhi
ya mambo, nisingependa kuliongelea kwa sababu kuna baadhi ya vitu
ambavyo wameviharibu sana, na hawakuweza kuviweka sawa,” alisema Idris.
Aliongeza, “Yaani kama kupunyua, hivi vitu vinatokeaga katika sehemu
yoyote, kwenye kampuni, kwenye nini. Kuna watu wanaweza wakafuja mali
zako au wakafanya vitu vibaya kinyume na mlivyo kubaliana. Kwa hiyo siyo
inshu kubwa sana kwangu, kwa sababu maisha yanaendelea na milango
inafunguka,”
Stori ambazo zilikuwa katika mitandao ya kijamii zilikuwa zinadai
kuwa meneja wa zamani wa Idris, ndiye ambaye alimwingiza mkenge Idris,
kitu ambacho Idris hakupenda kukizungumzia zaidi.
Pia Idris amesema kwa sasa amepata menejimenti mpya ambayo itakuwa inamwongoka katika kazi mbalimbali
0 comments:
Post a Comment