Saturday 14 May 2016

PICHA:29:YANGA FC BAADA YA KUKABIDHIWA KOMBE LA LIGI KUU TANZANIA BARA ZIKO HAPA.

 Timu Yanga kupewa Kombe Baada ya mchezo wao na NDANDA kumalizika na kutoka sale ya mbili kwa mbili.

May 14, 2016 ni siku ambayo Yanga imekabidhiwa kombe la ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu wa 2015-16 baada ya kufanya vizuri kwenye mechi zake na kujihakikishia pointi za kutosha ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ndani ya VPL.

Ni historia ya aina yake kwa mashabiki na wanachama, wachezaji, benchi la ufundi pamoja na uongozi kwa ujumla kwani ni kitu ambacho waliwekeza muda, pesa na kila kitu ili kuhakikisha wanafanikiwa kuwa mabingwa.

Miongoni mwa vitu vya kuvutia katika sherehe za Yanga kukabidhiwa kombe lao ni namna ambavyo baadhi ya wachezaji walivyojumuika kushangilia ubingwa huo wakiwa na familia zao pamoja na watu wao wa karibu.

Hizi hapa picha za matukio mbalimbali yaliyojiri wakati sherehe za Yanga kukabidhiwa mwali wao wa 26 katika historia ya klabu hiyo kwenye ligi kuu ya soka Tanzania bara.


 Waziri wa Mifugo, Kilimo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba akiikabidhi Yanga Kombe la Ligi Kuu mapema leo kwenye uwanja wa taifa jijini Dar, timu hiyo imecheza na Ndanda FC na matokeo 2-2. Huu ni ubingwa wa 26.
 Timu ya Yanga Fc yakabidhiwa Kombe hii leo baada ya mchezo wake na NDANDA.Ongera sana Timu ya Yanga Fc kuwa mabingwa wa Tanzania bara.

0 comments:

Post a Comment