Thursday, 30 June 2016

#YALIYOJIRI>>>>>Waziri Mkuu awataka wabunge wa upinzani kurejea Bungeni.Fahamu zaidi hapa.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa leo, Bungeni Mjini Dodoma amewataka wabunge wa upinzani ambao wamesusia vikao vya Bunge tangu Mei 30 kuingia Bungeni na kuacha kususia vikao vya Bunge kwani hakuna tija kwa Taifa.

Mhe. Majaliwa ameyasema hayo alipokuwa akitoa hutuba ya kuhitimisha mkutano wa tatu wa Bunge la kumi na moja.

“Kitendo cha baadhi ya waheshimiwa wabunge kususia vikao vya Bunge hakitoi picha nzuri kwa wananchi waliotuchagua kuwasilisha matatizo yao katika Bunge hili, hivyo natoa rai kwa waheshimiwa wabunge hao kutafakari upya uamuzi wao na niwasihi kwa busara zao waingie ili kwa pamoja na kwa ushirikiano tuweze kutoa ushauri kwa Serikali,” alisema Mhe. Majaliwa.

Aidha Mhe. Majaliwa alitoa ufafanuzi juu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambayo imetoa haki na kinga kwa waheshimiwa wabunge ili kujadili na kuhoji utendaji wa Serikali kwa uhuru bila mashaka yoyote ya kuweza kushitakiwa wanapotimiza wajibu wao wakiwa Bungeni.

Aliendelea kwa kusema kuwa kinga ya aina hiyo haijatolewa kwa mwananchi yeyote yule Nchini ila kwa Wabunge, hivyo basi hakuna mbunge aliyefungwa mdomo labda aamue kujifunga mdomo yeye mwenyewe.

Mhe. Majaliwa amesema kuwa Bunge linaongozwa na Katiba, Sheria na Kanuni za Kudumu za Bunge, hivyo ni vyema zikafuatwa kuondoa manung’uniko yasiyo ya lazima na endapo kuna utata katika jambo lolote ndani ya Bunge zipo taratibu zilizowekwa na kanuni za kufuata ili kupata ufumbuzi na si kwa kususa kuingia Bungeni kwani hakuna tija kwa Taifa.

Wabunge wa upinzani wamesusia vikao vya Bunge tangu Mei 30, 2016 mpaka leo Juni 30 ambapo Bunge limehitimishwa.

Aidha wabunge hao wamekuwa wakiingia Bungeni kila asubuhi na jioni kisha kutoka mara tu Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson anapomaliza kusoma Dua maalum la kuliombea Bunge na Taifa.

Sunday, 26 June 2016

Diamond Platnumz akosa tena Tuzo ya BET…Huyu ndie Mshindi wa Tuzo hii.Fahamu zaidi hapa.

Tuzo za BET katika kipengele cha Best Internation Act-Africa zimeshatolewa tayari na tuzo hii imeenda kwa Black Coffee.
Katika Tuzo hii Black Coffee alikuwa akishindina vikali na wababe wa Muziki wa Afika kwa sasa akiwemoDiamond Platnumz, Wizkid, Yemi Alade na Cassper Nyovest kutoka nchini Afrika ya kusini.
HUYU NDIE BLACK COFFEE

Katika Mtandao wa Instagram wa BET AFRIKA wamepost picha ya Black Coffee na kuandika “🎉🎊 Winner: Best International Act: Africa – Black Coffee #BETAwards16“.
 
Bahati haikuwa kwetu, Hongera Pia kwa Diamond Platnumz japo hajashinda lakini ametuwakilisha vizuri sana katika kuufikisha Muziki wetu katika level ya Kimataifa.

Breaking News>>>>Rais Magufuli Afanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya na Afanya Mabadiliko Madogo ya Wakuu wa Mikoa.Fahamu zaidi hapa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya mabadiliko madogo katika safu ya wakuu wa mikoa na amewateua wakuu wa wilaya 139.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika mabadiliko hayo Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Bi. Zainab R. Telack kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Bi. Zainab R. Telack anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Anna Kilango Malecela ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Rais Magufuli pia amemteua Dkt. Binilith Satano Mahenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.

Dkt. Binilith Satano Mahenge anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabit Mwambungu ambaye amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es salaam ambako atapangiwa majukumu mengine.

Aidha, Rais Magufuli amemteua Dkt. Charles F. Mlingwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Dkt. Charles F. Mlingwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Stanslaus Magesa Mulongo ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Wakuu wapya wa mikoa walioteuliwa wataapishwa tarehe 29 Juni, 2016 saa tatu kamili asubuhi Ikulu Jijini Dar es salaam na mara baada ya kuapishwa watakula kiapo cha maadili ya uongozi.
 
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya 139.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika uteuzi huo Rais Magufuli amezingatia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na umri ambapo kwa wale ambao umri wao ni zaidi ya miaka 60 ameamua wastaafu.

Mhe. Rais amewashukuru sana kwa utumishi wao mzuri na amesema pale ambapo itahitajika, serikali itaendelea kuwatumia katika majukumu mengine.

Katika uteuzi huo, Wakuu wa Wilaya waliopo sasa ambao wamebaki katika nafasi zao ni 39. Pia Rais Magufuli amewateua Wakurugenzi Watendaji wa halmashauri 22 kuwa Wakuu wa Wilaya kutokana na utendaji wao mzuri.

Aidha, nafasi 78 za uteuzi wa Wakuu wa wilaya zimejazwa na watanzania wengine ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza wengi wao wakiwa ni vijana, wenye elimu ya kutosha na uzoefu katika maeneo mbalimbali

Walioteuliwa kuwa wakuu wa wilaya ni kama ifuatavyo (Orodha imepangwa kulingana na mikoa)
ARUSHA
  1. Arusha           -           Mrisho Mashaka Gambo
  2. Arumeru        -           Alexander Pastory Mnyeti
  3. Ngorongoro  -           Rashid Mfaume Taka
  4. Longido         -           Daniel Geofrey Chongolo
  5. Monduli         -           Idd Hassan Kimanta
  6. Karatu                        -           Therezia Jonathan Mahongo


DAR ES SALAAM
  1. Kinondoni     -           Ally Hapi
  2. Ilala                -           Sophia Mjema
  3. Temeke         -           Felix Jackson Lyaviva
  4. Kigamboni     -           Hashim Shaibu Mgandilwa
  5. Ubungo          -           Hamphrey Polepole

DODOMA
  1. Chamwino     -           Vumilia Justine Nyamoga
  2. Dodoma        -           Christina Solomon Mndeme
  3. Chemba         -           Simon Ezekiel Odunga
  4. Kondoa          -           Sezeria Veneranda Makutta
  5. Bahi                -           Elizabeth Simon
  6. Mpwapwa      -           Jabir Mussa Shekimweli
  7. Kongwa          -           John Ernest Palingo

GEITA
  1. Bukombe      -           Josephat Maganga
  2. Mbogwe         -           Matha John Mkupasi
  3. Nyang'wale     -           Hamim Buzohera Gwiyama
  4. Geita               -           Herman C. Kipufi
  5. Chato             -           Shaaban Athuman Ntarambe

IRINGA
  1. Mufindi          -           Jamhuri David William
  2. Kilolo             -           Asia Juma Abdallah
  3. Iringa              -           Richard Kasesela

KAGERA
  1. Biharamulo   -           Saada Abraham Mallunde
  2. Karagwe         -           Geofrey Muheluka Ayoub
  3. Muleba          -           Richard Henry Ruyango
  4. Kyerwa           -           Col. Shaban Ilangu Lissu
  5. Bukoba          -           Deodatus Lucas Kinawilo
  6. Ngara             -           Lt. Col. Michael M. Mtenjele
  7. Missenyi         -           Lt. Col Denis F. Mwila

KATAVI
  1. Mlele              -           Rachiel Stephano Kasanda
  2. Mpanda         -           Lilian Charles Matinga
  3. Tanganyika    -           Saleh Mbwana Mhando

KIGOMA
  1. Kigoma           -           Samsoni Renard Anga
  2. Kasulu                        -           Col. Martin Elia Mkisi
  3. Kakonko       -           Col. Hosea Malonda Ndagala
  4. Uvinza                        -           Mwanamvua Hoza Mlindoko
  5. Buhigwe         -           Col. Elisha Marco Gagisti
  6. Kibondo        -           Luis Peter Bura

KILIMANJARO
  1. Siha                -           Onesmo Buswelu
  2. Moshi             -           Kippi Warioba
  3. Mwanga         -           Aaron Yeseya Mmbago
  4. Rombo           -           Fatma Hassan Toufiq
  5. Hai                 -           Gelasius Byakanwa
  6. Same              -           Rosemary Senyamule Sitaki

LINDI
  1. Nachingwea   -           Rukia Akhibu Muwango
  2. Ruangwa        -           Joseph Joseph Mkirikiti
  3. Liwale             -           Sarah Vicent Chiwamba
  4. Lindi               -           Shaibu Issa Ndemanga
  5. Kilwa              -           Christopher Emil Ngubiagai


MANYARA
  1. Babati             -           Raymond H. Mushi
  2. Mbulu                        -           Chelestion Simba M. Mofungu
  3. Hanang'         -           Sara Msafiri Ally
  4. Kiteto              -           Tumaini Benson Magessa
  5. Simanjiro       -           Zephania Adriano Chaula

MARA
  1. Rorya              -           Simon K. Chacha
  2. Serengeti        -           Emile Yotham Ntakamulenga
  3. Bunda                        -           Lydia Simeon Bupilipili
  4. Butiama         -           Anarose Nyamubi
  5. Tarime           -           Glodious Benard Luoga
  6. Musoma        -           Dkt. Vicent Anney Naano

MBEYA
  1. Chunya          -           Rehema Manase Madusa
  2. Kyela              -           Claudia Undalusyege Kitta
  3. Mbeya                        -   William Ntinika Paul
  4. Rungwe          -           Chalya Julius Nyangidu
  5. Mbarali          -           Reuben Ndiza Mfune

MOROGORO
  1. Gairo              -           Siriel Shaid Mchembe
  2. Kilombero     -           James Mugendi Ihunyo
  3. Mvomero       -           Mohamed Mussa Utali
  4. Morogoro      -           Regina Reginald Chonjo
  5. Ulanga                        -           Kassema Jacob Joseph
  6. Kilosa             -           Adam Idd Mgoyi
  7. Malinyi           -           Majula Mateko Kasika

MTWARA
  1. Newala           -           Aziza Ally Mangosongo
  2. Nanyumbu    -           Joakim Wangabo
  3. Mtwara           -           Dkt. Khatibu Malimi Kazungu
  4. Masasi                        -           Seleman Mzee Seleman
  5. Tandahimba -           Sebastian M. Walyuba

MWANZA
  1. Ilemela           -           Dkt. Leonald Moses Massale
  2. Kwimba          -           Mhandisi Mtemi Msafiri Simeon
  3. Sengerema     -           Emmanuel Enock Kipole
  4. Nyamagana    -           Mary Tesha Onesmo
  5. Magu              -           Hadija Rashid Nyembo
  6. Ukerewe        -           Estomihn Fransis Chang'ah
  7. Misungwi       -           Juma Sweda

NJOMBE
  1. Njombe          -           Ruth Blasio Msafiri
  2. Ludewa                      -           Andrea Axwesso Tsere
  3. Wanging'ombe          -           Ally Mohamed Kassige
  4. Makete                       -           Veronica Kessy

PWANI
  1. Bagamoyo      -           Alhaji Majid Hemed Mwanga
  2. Mkuranga      -           Filberto H. Sanga
  3. Rufiji               -           Juma Abdallah Njwayo
  4. Mafia              -           Shaibu Ahamed Nunduma
  5. Kibaha           -           Asumpter Nsunju Mshama
  6. Kisarawe        -           Happyness Seneda William
  7. Kibiti               -           Gulamu Hussein Shaban Kifu

RUKWA
  1. Sumbawanga -           Dkt. Khalfan Boniface Haule
  2. Nkasi              -           Said Mohamed Mtanda
  3. Kalambo        -           Julieth Nkembanyi Binyura

RUVUMA
  1. Namtumbo    -           Luckness Adrian Amlima
  2. Mbinga           -           Cosmas Nyano Nshenye
  3. Nyasa             -           Isabera Octava Chilumba
  4. Tunduru        -           Juma Homela
  5. Songea           -           Polet Kamando Mgema

SHINYANGA
  1. Kishapu         -           Nyambonga Daudi Taraba
  2. Kahama         -           Fadhili Nkulu
  3. Shinyanga      -           Josephine Rabby Matiro

SIMIYU
  1. Busega           -           Tano Seif Mwera
  2. Maswa                        -           Sefu Abdallah Shekalaghe
  3. Bariadi           -           Festo Sheimu Kiswaga
  4. Meatu             -           Joseph Elieza Chilongani
  5. Itilima             -           Benson Salehe Kilangi

SINGIDA
  1. Mkalama       -           Jackson Jonas Masako
  2. Manyoni        -           Mwembe Idephonce Geofrey
  3. Singida           -           Elias Choro John Tarimo
  4. Ikungi             -           Fikiri Avias Said
  5. Iramba           -           Emmanuel Jumanne Luhahula

SONGWE
  1. Songwe           -           Samwel Jeremiah
  2. Ileje                -           Joseph Modest Mkude
  3. Mbozi             -           Ally Masoud Maswanya
  4. Momba          -           Juma Said Irando


TABORA
  1. Nzega             -           Geofrey William Ngudula
  2. Kaliua             -           Busalama Abel Yeji
  3. Igunga                        -           Mwaipopo John Gabriel
  4. Sikonge          -           Peres Boniphace Magiri
  5. Tabora           -           Queen Mwashinga Mlozi
  6. Urambo         -           Angelina John Kwingwa
  7. Uyui                -           Gabriel Simon Mnyele

TANGA
  1. Tanga             -           Thobias Mwilapwa
  2. Muheza          -           Mhandisi Mwanaisha Rajab Tumbo
  3. Mkinga           -           Yona Lucas Maki
  4. Pangani          -           Zainab Abdallah Issa
  5. Handeni        -           Godwin Crydon Gondwe
  6. Korogwe        -           Robert Gabriel
  7. Kilindi                        -           Sauda Salum Mtondoo
  8. Lushoto         -           Januari Sigareti Lugangika
Wakuu wote wa Wilaya walioteuliwa wanapaswa kufika Ikulu Dar es salaam siku ya Jumatano tarehe 29 Juni, 2016 saa tatu kamili asubuhi kwa ajili ya kiapo cha maadili ya uongozi na maelekezo mengine kabla ya kuapishwa na wakuu wa mikoa watakaporejea katika mikoa yao.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
26 Juni, 2016

#MICHEZO>>>KUELEKEA MECHI NA TP MAZEMBE,WAKONGWE WAIPA YANGA MBINU.Fahamu zaidi hapa.

WACHEZAJI wa zamani wa Yanga na Simba wameitaka Yanga kutobweteka katika mchezo ujao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe na badala yake watulie na kutumia vyema uwanja wa nyumbani kupata matokeo mazuri.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti , wachezaji hao walisema Yanga ilionesha kandanda nzuri katika mchezo dhidi ya Mo Bejaia isipokuwa safu ya ushambuliaji haikucheza kwa utulivu.
Miongoni mwa wachezaji hao ni Mwanamtwa Kihwelu na Moses Mkandawile waliosema kuwa Yanga inaweza kupata matokeo mazuri iwapo kama hawatabweteka, na ikiwa watapambana kwa ushirikiano.

Kihwelu alisema: “TP Mazembe sio timu nyepesi kwani ina uzoefu wa mashindano hayo, na tayari wana pointi tatu na kuhimiza Yanga kutulia kwenye uwanja wa nyumbani kutengeneza nafasi zenye kuzaa matunda.”

Alisema kinachohitajika ni mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara kuzidisha mara mbili kiwango chao ili kuwa na uhakika wa kuibuka na ushindi. Kihwelu alipendekeza kuwa iwapo Juma Abdul na mchezaji mpya Obrey Chirwa watakuwepo kuna uwezekano wa kupata ushindi mzuri.

Kwa upande wake, Mkandawile aliwahimiza Yanga kucheza wakijua kuwa wako kwenye uwanja wa nyumbani. Alisema ni muhimu kuzingatia nidhamu kwa ajili ya kuepukana na kadi nyingi zisizokuwa na tija .

Golikipa huyo wa zamani wa Simba alisema sehemu inayohitaji kufanyiwa kazi ni safu ya ulinzi na ushambuliaji, kwani wanahitaji kucheza kwa utulivu mkubwa. Yanga wanatarajiwa kushuka dimbani Juni 28, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa pili hatua ya makundi. Kwa sasa wanaendelea kujifua na mazoezi katika kambi yao iliyoko nje ya nchi Uturuki na kesho wanatarajiwa kurudi.

Saturday, 25 June 2016

#MICHEZO>>>>Euro2016: Poland yailaza Switzerland.Fahamu zaidi hapa.

 Lewandowski 
 
Poland itakutana na Croatia ama Portugal katika robo fainali ya michuano ya Euro2016 baada ya kuishinda Switzerland kwa Penalti.

Jakub Blaszczykowski aliiweka mbele Switzerland kabla ya Xherdan Shaqiri kusawazisha kupitia bao zuri.
 Mashabiki wa Poland 
 
Mchezaji huyo wa Stoke alimfunga Lukas fabianski kupitia shambulio la 'Bycycle kick' kwa lugha ya Kiingereza.
Poland wakisherehekea bao lao 
 
Mchezaji aliyesajiliwa hivi majuzi na klabu ya Arsenla Granit Xhaka alikosa penalti kwa upande wa Switzerland baada ya mechi hiyo kuisha na sare ya 1-1.

#YALIYOJIRI>>>>Mafuriko yawaua watu 20 Marekani.Fahamu zaidi hapa.

Mafuriko Marekani 
Zaidi ya watu 20 wamefariki kutokana na mafuriko makubwa yaliyokumba jimbo la magharibi la Virginia.
Gavana wa jimbo hilo amesema mafuriko hayo yamesababisha hasara kubwa huku majumba karibu elfu 60 yakikatiziwa umeme.

Imebidi baadhi ya watu kuokolewa ,kutoka mapaa ya majumba walikotorokea mafuriko hayo.

Kinaya ni kuwa upande mwengine wa nchi hiyo hasa katika jimbo la California hali ya kiangazi na joto jingi imesababisha mioto .

Katika eneo hilo watu wawili wamefariki huku wengine mamia wakilazimika kuyahama makaazi yao.

Chanzo:BBC SWAHILI.

#MICHEZO>>>Croatia yafa Kwa counter attack moja ya dakika za mwishon ndan ya extra time.Fahamu zaidi hapa.

 Ricardo Quaresma akifunga goli kwa kichwa aliloshinda dakika za niongeza.

Renato Sanches,miaka mwenye umri wa miaka 18 ambae anawindwa na Bayern Munich kukubali kutumià pesa ya kuweka rekodi ya usajili kwa kinda huyu,haikuwa jambo,dogo kufunga goli...Sub yake na Ricardo Quaresma imejibu,tena lala salama.

Croatia lazima wajilaumu,wametengeneza nafasi nyingi mno za kufunga,kuliko Portugal lakini ni sawa na kusema 'badluck'...Counter attack imewaondoa moja kati ya timu iliyoonyesha kuwa timu bora iwapo uwanjani ikionekana inacheza soka la hali ya juu sana kwenye Euro hii...Ila kinachofulahisha kumuona 'fundi' Sanches kwa mechi nyingine moja,kama sio tatu...Dogo aliikataa ofa ya Man United,akaikubali Bayern kuwa ni timu itakayompa mataji.Sanches yupo vizuri,Sana tu.

Huku Cristiano Ronaldo aweka rekodi kwa michezo 128 na kumpita Luis Figo kwa kuichezea timu ya taifa michezo mingi zaidi.
 Ricardo Quaresma akishangilia goli aliloshinda dakika za niongeza.
HILI NDILO GOLI WALILOSHINDI "Portugal"

#Breaking News>>>>Orodha Ya Majina Ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Na Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Ufundi Kwa Mwaka 2016.Fahamu zaidi hapa.

OR-TAMISEMI inawatangazia majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2016. 
Wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka shule za Serikali na zisizo za Serikali. Jumla ya wanafunzi 65,720 wakiwemo wasichana 29,457 na wavulana 36,263 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi. 
Kati ya wanafunzi waliochaguliwa 34,064 wakiwemo wasichana 13,466 na wavulana 20,598 sawa na asilimia 52 watajiunga na masomo ya Sayansi na Hisabati; na wanafunzi 30,897 wakiwemo wasichana 15,445 na wavulana 15,452 sawa na asilimia 47 wamechaguliwa kusoma masomo ya Sanaa na Biashara na wanafunzi 759 wakiwemo wasichana 220 na wavulana 539 sawa na asilimia 1 wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya Ufundi.

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2016 wataanza muhula wa kwanza tarehe 11 Julai, 2016 na hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya shule. 

Wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti hadi tarehe 24 ambayo ndiyo siku ya mwisho ya kuripoti, nafasi yake itachukuliwa na mwanafunzi mwingine aliyekosa nafasi.

Imetolewa na Katibu Mkuu,
OR-TAMISEMI

Tumia link hii kupata matokeo Waliochaguliwa kidato cha tano na vyuo vya ufundi 2016


#YALIYOJIRI>>>Serikali Yasitisha Tamko la Utoaji wa Chakula Muhimbili.Fahamu zaidi hapa.

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto , imesitisha tamko la utoaji wa vyakula kwa wagonjwa watakaolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kupisha utafiti wa kina kuhusu huduma hiyo ili kuweza kutoa kilicho bora kwa watanzania.

Akizungumza hayo leo jijini Dar es salaam Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Ummy Mwalimu amesema kwamba wameamua kusitisha mpango mpaka watapotangaza tena ili kufanya utafiti kujua kama kuna faida au hasara kwa wananchi.

“Natoa tamko kwamba huduma hii iliyotarajiwa kuanza hivi karibuni isitishwe mara moja ili kupisha watafiti waweze kufanya uchunguzi kujua inawasaidia kwa kiasi gani wananchi” alisisitiza Bi. Mwalimu.

Aidha Bi. Mwalimu amesema kwamba huduma hiyo itatolewa kwa wagonjwa watakaolazwa hapo kwa kulipia shilingi elfu 50 ikiwemo shilingi elfu kumi ya kumuona daktari , elfu kumi ya kitanda na elfu 30 iliyobaki ni kwa malipo ya chakula kwa wiki.

“Huduma hii inalenga kuwasaidia wananchi katika kuwaandalia chakula stahiki kwa wagonjwa na kupunguza usumbufu kwa waangalizi wa wagonjwa wao kuleta vyakula hospitalini ili kuimalisha afya zao kwa ujumla” aliongeza Bi.Mwalimu.