Tuesday, 7 June 2016

#‎MICHEZO‬>>>SERIKALI UCHAGUZI WA YANGA NI BATILI.Fahamu zaidi hapa.

WAKATI uongozi wa Yanga umewasilisha ripoti ya tuhuma za rushwa kwenye Taasisi ya Kupambana na Rushwa (Takukuru), Serikali imesisitiza kuwa haitambui mchakato wa uchauguzi unaoendelea ndani ya klabu hiyo.

Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Mohamed Kiganja alisema kuwa BMT haiungi mkono kinachoendelea ndani ya Yanga kwa vile ni kinyume cha Katiba. “Kinachofanyika Yanga kwa sasa ni uvunjifu wa Katiba, kama Serikali hatuungi mkono, “alisema Kiganja kwa kifupi. Kiganja ambaye wiki iliyopita pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Shirikisho la Soka Tanzania, Aloyce Komba walituhumiwa na Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kuwa walihusika katika uvurugaji wa uchaguzi huo.


Komba baada ya tuhuma hizo alitangaza kujiweka kando kushughulikia.

0 comments:

Post a Comment