Rapper kutoka Tanzania, Nay wa Mitego amejikuta matatani baada ya kutua mikoni mwa Jeshi la Polisi na kuhojiwa kufuatia tuhuma zinazomkabili na baadaye kuachiwa kwa dhamana.

Kamanda wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro amethibitisha kuwa msanii huyo alihojiwa lakini hakueleza ni makosa gani yanayomkabili. Aidha Kamanda Simon Sirro alisema kuwa wanakamilisha taratibu na taarifa kamili itatolewa siku ya Jumatatu.

Watu tofauti wamekuwa wakisema kuwa huenda mwanamuziki huyo ametua mikononi mwa polisi kufuatia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la “Pale kati patamu” ambapo cover la wimbo huo, wanaonekana wadada waliko uchi.