Home »
Michezo
» #MICHEZO>>>MATERAZZI AMEONGEA KWA MARA YA KWANZA ILE ISHU YA KUPIGWA KICHWA NA ZIDANE.Fahamu zaidi hapa.
Marco Materazzi kwa mara ya kwanza ametanabaisha kile alimwambia
Zinedine Zidane kabla ya kupigwa kichwa kwenye fainali ya Kombe la Dunia
mwaka 2006. Vile vile amekiri kwamba tukio lile lilibadilisha kabisa
mfumo wa maisha yake baada ya kuanza kufuatiliwa kwa karibu sana vyombo
vya habari.
“Tangu siku ile, nilianza kuombwa kufanya mahojiano na vyombo
mbalimbali duniani. ” Materazzi aliongea na L’Equipe (kupitia gazeti la
Marca).
“Niliamua kuchapisha kitabu juu ya tukio lile kwa sababu kila mtu
alikuwa akiniuliza ni kitu gani hasa nilimwambia Zidane kiasi cha
kufikia hatua ya kufanya tukio lile. Maneno hayakuwa mazuri lakini hata
hivyo sikupaswa kuhukumiwa kwa namna ile. Kwenye maeneo mengi
ninayoyafahamu kama Rome, Naples, Turin, Milan Paris, huwa nasikiga
zaidi hata ya nilichomwambia, ” aliongeza.
“Mimi nilimzungumzia dada yake na wala sio mama yake, kama ambavyo
nimesoma kwenye baadhi ya magazeti. Mama yangu alikufa nikiwa kijana
mdogo sana, hivyo isingekuwa rahisi kwangu kutukana tusi hilo.”
Marco Materazzi alienda mbali zaidi na kusema kwamba haelewi kwanini stori ile ilipaishwa sana na vyombo vya habari namna ile.
“Sijui kwanini stori ile iliwekwa chumvi kiasi kile. Kitu pekee
ambacho naweza kukumbuka kutoka kwenye fainali ile ni magoli yangu
mawili niliyofunga.”
Related Posts:
Mbeya City Waisafishia Njia Yanga Njia ya Ubingwa.Fahamu zaidi hapa.
Mbeya City wamaliza mchezo, kazi kwenu Yanga
KLABU ya Simba imeng’ang’aniwa na Mbeya City huku ikilazimishwa sare
kutoka sare ya bao 2-2, katika mchezo uliopigwa leo kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar.
Mbeya City ndiyo w… Read More
MAN UTD KUAMUA HATMA YA MICHAEL CARRICK.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Kiungo Michael Carrick ameahidi kustaafu soka, endapo uongozi wa Man
Utd utasitisha mpango wa kumsainisha mkataba mpya mwishoni mwa msimu
huu.
Carrick mwenye umri wa miaka 35, amekua Old Trafford tangu Julai 2006
akitok… Read More
Samatta kaifungia KRC Genk goli mbili vs Club Brugge katika ushindi wa 2-1 (+Video).Fahamu zaidi hapa.
Usiku wa March 4 2017 nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta aliingia katika uwanja wao wa nyumbani wa Luminus Arena kuitumikia club yake ya KRC Genk katika mchezo wa Ligi Kuu Ubelgiji dhidi y… Read More
Hali ya uchumi Yaifanya Yanga Kuachana na Hans Pluijm...!!.Fahamu zaidi hapa.
Matatizo ya kiuchumi yanayoikabili Yanga, yamesababisha timu hiyo kuachana na mkurugenzi wake wa ufundi, Hans Pluijm.
, Pluijm amethibitisha kupokea barua kutoka kwa uongozi wa timu hiyo ambao umeamua kuachana naye ili … Read More
LIVERPOOL YAINYOOSHA ARSENAL 3-1 NA KUIONDOA TOP FOUR.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Liverpool: Mignolet, Clyne, Matip, Klavan, Milner, Wijnaldum, Can, Lallana, Mane, Firmino, Coutinho (Origi 79)
Subs not used: Karius, Lovren, Moreno, Lucas, Woodburn, Alexander-Arnold
Goalscorers: Firmino 9, Mane… Read More
0 comments:
Post a Comment