Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini, limekifutia
usajili wake wa kutoa huduma za kitabu, Kituo cha Tiba Asilia cha
ForePlan Kliniki iliyopo Ilala Bungoni jijini Dar es salaam,
kinachomilikiwa na Dkt. Juma Mwaka maarufu kama Dkt. Mwaka, kwa madai
kuwa kimekiuka taratibu za kitabu za tiba asili huku akiwa ameonywa na
kushindwa kubadilika.
Akizungumza jijini Dar es salaam leo katika Mkutano na
waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dk. Edmund Kayombo
amesema kuwa kufutiwa kibali cha Dk. Mwaka kunatokana na sababu nyingi
ambazo amekuwa akikiuka licha ya kupewa maonyo na barua juu ya utoaji
huduma zake.
Amesema sababu nyingine ni kuwa katika matangazo yake amesema anatoa tiba za kisasa wakati hiyo elimu hana ya kufanya hivyo.
Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba
Mbadala , Dk. Edmund Kayombo akizungumza na waandishi habari juu hatua
walizozichukua kwa watoaji huuduma tiba asili na tiba mbadala leo jijini
Dar es Salaam, kulia ni Msajili Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala,
Ruth Suza kushoto ni Kaimu Mkurugenz Msaidizi wa Huduma na Tiba Mbadala,
Paulo Muhame.
Wengine waliofutiwa usajili ni Fadhaget Sanitarium
kinachoendeshwa na Tabibu Fadhili Kabujanja pamoja na Mandai Herbal
Clinic kinachoendeshwa na Tabibu Abdallah Mandai
Hata hivyo limetoa adhabu mbalimbali kwa kituo cha Aman
Herbal Clinic kinachoendeshwa na Tabibu Esbon Baroshigwa, na Tabibu
Castory Ndulu wa Kituo cha Ndulu Herbal Clinic wamepewa barua ya onyo.
Aidha wengine wamesimashwa kwa miezi sita ambao ni Tabibu
John Lupimo wa Lupimo Suntarium Herbal Clinic pamoja na Tabibu Simon
Rusigwa wa Sigwa Herbal Clinic.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma na
Tiba Mbadala, Paulo Muhame akizungumza na waandishi habari juu ya
utekelezaji wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto kwa wanaokiuka taratibu za utoaji huduma wa tiba asili na tiba
mbadala katikati ni Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala ,
Dk. Edmund Kayombo kulia ni Msajili Baraza la Tiba Asili na Tiba
Mbadala, Ruth Suza.
Dk. Kayombo amesema kuwa wale wote ambao wamepewa onyo pamoja
na kusimamishwa wametakiwa wasiingie mikataba na vyombo vya habari kwa
ajili ya Matangazo
Amesema kuwa waliofutiwa walifuata taratibu zote ikiwa
kuwahoji na kujiridhisha kuwafutia kibali cha utoaji wa huduma za tiba
asili na tiba mbadala.Imeandikwa na Chalila Kibuda.
0 comments:
Post a Comment