MAMLAKA ya Udhibiti ya Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema kuna akiba ya kutosha ya mafuta ya aina mbalimbali yanayoweza kutumika kati siku 13 hadi 39 nchini.
Mkurugenzi
Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi, alisema hayo jijini Dar es Salaam jana
katika mkutano na wadau wa sekta ya mafuta nchini wa kupokea maoni juu
ya mfumo wa uingizaji wa mafuta nchini.
Tamko
la EWURA limekuja kukiwa na tatizo la uhaba wa mafuta ya petrol, dizeli
na mafuta ya taa katika baadhi ya mikoa hali iliyosababisha wananchi wa
mikoa iliyokumbwa na tatizo hilo kupata adha.
Ngalamgosi
alisema akiba ya mafuta ya ndege iliyopo inatosha kutumika kwa siku 30
kwa nchini nzima, petroli ni zaidi ya siku 12, dizeli ni zaidi ya siku
15, mafuta ya taa ni zaidi ya siku 16, mafuta ya viwandani ni zaidi ya
siku 39 na mafuta ya migodini zaidi ya siku 13.
Alisema
sababu ya kutokea uhaba wa mafuta unaoonekana sasa ni kuwepo kwa
sikukuu zilizofululiza na kusababisha magari ya kubeba mafuta kushindwa
kusafirisha mafuta, na ama kufika kwa wakati katika mikoa hiyo
iliyokubwa na kadhia hiyo.
Jumatano na Alhamisi zilizopita palikuwa na siku kuu za Eid el Fitri.
“Niwaombe
Watanzania wawe na subira kwani mafuta yapo yakutosha, hivyo nawaomba
wasinunue mafuta kwa kupaniki kwani magari ya kusafirisha mafuta
yameanza kusambaza katika mikoa hiyo na hali itatulia kuanzia sasa,” alisema.
Alisema
magari ya mafuta yameshapeleka shehena katika mikoa ya Mtwara, Ruvuma,
Songea na Mbinga ambako hali ya upatikanaji wa mafuta imeanza kutulia.
Mafuta ya taa
Ngalamgosi
alisema uhaba wa mafuta ya taa ulitokana na meli iliyokuwa ikishusha
mafuta ya ndege na petroli kuyachaganya wakati wa kuyasukuma.
Alisema
kuwa kutokana na mchanganyiko huo ni wazi kuwa mafuta ya ndege ambayo
ndio hutumika kama mafuta ya taa, hayaweza kutumika kwa matumizi ya
kawaida.
“Mafuta
ya ndege ndio hayo hayo yanatumika kama mafuta ya taa hivyo kutokana na
kuchanganyika huko ilipaswa kusafisha matanki yote na mabomba ili
kuweka mafuta mapya,” alisema.
Alisema
zoezi la kuyasafisha matanki matano lilifanyika kwa wiki tatu mfululizo
na kukamilika Julai 2, kabla ya kuanza kupokea mafuta na kuyasambaza
Julai 3 mwaka huu katika mikoa ambayo kulitokea uhaba.
Kampuni za ndani
Ngalamgosi
alisema EWURA imependekeza kubadilishwa kwa mfumo wa uingizwaji wa
mafuta nchini kutoka nchini za nje kwa kuanzishwa mfumo mpya wa kutoa
fursa kwa kampuni za ndani kuingiza mafuta nchini.
Ngalamgosi
alisema kuwa amekutana na wadau wa sekta ya mafuta ili kupokea maoni ni
namna gani wanaweza kuboresha ushindani na wamependekeza kuwa kila meli
inayokuja lazima iwe na zabuni yake.
Alisema
Tanzania inaingiza meli sita za mafuta kwa mwezi, hivyo EWURA imeona
kuwa inapasa kuwa kila meli ya mafuta inayoingia iwe zabuni
inayojitegemea.
“Kwa
kufanya hivyo kutatoa fursa kwa watanzania kuweza kuingiza mafuta kwa
sababu itapunguza gharama na uzuri utakuwa nchi itanufaika kuwa na
watanzania wengi kushiriki katika kuingiza mafuta,”alisema.
Aliongeza kuwa kupita utaratibu mpya wanaamini kuwa makampuni ya Tanzania yatapata faida kubwa na TRA kukusanya mapato mengi.
0 comments:
Post a Comment