Home »
Habari Moto
» #YALIYOJIRI>>>>Jukwaa la Wahariri lapinga Mseto kufungiwa.Fahamu zaidi hapa.
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limepinga hatua ya Serikali kulifungia
gazeti la Mseto kwa mtindo wa yenyewe kujifanya mlalamikaji, mwendesha
mashtaka na hakimu.
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limepokea kwa mshituko taarifa za
kufungiwa kwa miezi 36 gazeti la Mseto kwa kutumia kifungu cha 25(1) cha
Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976.
Katika maelezo ya Waziri, Nape Nnauye anasema tangu Mwaka 2012 wamekuwa wakiwaonya Mseto bila gazeti hilo kubadilika.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Halihalisi, Saed Kubenea amekana kupata maonyo kutoka Serikalini.
Sisi TEF tunapinga utaratibu wa Serikali kuwa mlalamikaji, mwendesha mashitaka na Hakimu katika kesi inazohusika.
Tunataka mchakato wa kubadili Sheria ikaanzisha chombo cha kitaaluma cha
kusimamia wanahabari na vyombo vya habari uende haraka kwa nia ya
kumaliza kadhia hii.
Serikali imeahidi muda mrefu kubadili Sheria hii mbaya ya Magazeti lakini miaka yote utekelezaji umekuwa sifuri.
Tunasisitiza kuwa hatukubaliani na wala hatuungi mkono utaratibu huu wa Serikali kufungia au kufuta vyombo vya Habari.
Kwa upande mwingine tunapenda kuvitahadharisha vyombo vya Habari katika
matumizi ya nyaraka ili kuepuka kuingia katika migogoro na Serikali,
Jamii au mtu mmoja mmoja.
Pamoja na taarifa hii, TEF itafanya uchunguzi na uchambuzi wa adhabu
iliyotolewa kwa Gazeti la Mseto pamoja na habari iliyosababisha gazeti
hilo kufungiwa, kwa manufaa ya waandishi wa habari na vyumba vya habari.
Related Posts:
#YALIYOJIRI>>>BAKWATA Waunga Mkono Uchaguzi wa Marudio Zanzibar.Fahamu zaidi hapa.
WAKATI
Chama cha wananchi CUF ambacho ni chama kikuu cha Upinzani visiwani
Zanzibar kikiwa kimesusia uchaguzi wa marudio ambao unafanyika Marchi 20
ya mwaka huu,Baraza la Waislam (BAKWATA) limese… Read More
#YALIYOJIRI>>>Mke wa Kafulila Amlipua Dr. Mwakyembe Kuhusu Sakata La Mabehewa FEKI,Mwakyembe Akomaa, Asema Yupo Tayari Kujiuzulu Ikithibitika Fahamu zaidi hapa.
Sakata
la ununuzi wa mabehewa kwa ajili ya Shirika la Reli Tanzania (TRL)
yanayodaiwa kuwa mabovu liliibuka jana Bungeni na kumuinua Waziri wa
Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe ambaye alikuwa Waziri wa
Uchukuzi … Read More
#YALIYOJIRI>>>Afande Sele Aungana Na Mbunge Joseph Msukuma Kuitaka Serikali Ihalalishe Matumizi Ya Bhangi.Fahamu zaidi hapa.
Msanii
mkongwe wa hip hop nchini, Afande Sele amefunguka na kusema serikali
ihalalishe matumizi ya bangi na si kukosoa juu ya hoja iliyotolewa na
mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma.
Ikiwa
imepita siku moja t… Read More
#YALIYOJIRI>>>Zitto Kabwe Ang’ang’ania Ufisadi Benki ya Stanbic,Mwanasheria Mkuu Amshauri Apeleke Nyaraka Serikalini.Fahamu zaidi hapa.
MBUNGE
wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT- Wazalendo) ameitaka serikali
kumwagiza Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) ili kubaini
wizi wa Sh. 608 trilioni zilizokopwa kupitia Benki ya Stanbic yenye tawi
lake… Read More
#YALIYOJIRI>>>Bungeni: Serikali Kuajiri Vijana 71,408 Mwaka Huu,Halmashauri Zaagizwa Kutenga Asilimia 5 Ya Mapato Kwa Ajili Ya Kuwasaidia Vijana.Fahamu zaidi hapa.
Serikali
katika mwaka wa fedha 2016/2017 imepanga kuongeza ajira kwa vijana ili
kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana wengi wa
kitanzania kwa kuongeza ajira na kuwezesha wengine kujiajiri kupitia
mif… Read More
0 comments:
Post a Comment