Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm ameonekana kutofurahishwa na sare dhidi ya Ndanda FC mjini Mtwara, jana.
Yanga
imekwenda sare ya bila kufungana dhidi ya Ndanda kwenye Uwanja wa
Nangwanda Sijaona mjini Mtwara katika mchezo mzuri ambao ladha yake
ilipunguzwa na uwanja mbovu.
Habari kutoka ndani ya Yanga, Pluijm amewaeleza wacheaji wake kuchukizwa na sare hiyo.
“Lakini ameonyesha kutuamini, amesema lazima tubadili mambo na kushinda katika mechi zijazo,” alisema mmoja wa wachezaji.
0 comments:
Post a Comment