Na Dr Haroun Haroun
Yanga ina daktari wa timu anaitwa
Dr Edward bavu nafikiria ana taaluma ya kutibia wachezaj vizuri,
lakini wakati mwingine kwa sisi madaktari ikitokea ukishindwa kumtibu
mgonjwa unaweza kuomba daktari mwenzio akusaidie.
Nilipigiwa simu na Mjumbe mmoja wa
yanga ili nimsaidie kumtibu Donald Ngoma baada ya kutoka Zanzibar ,
Nilifanya hivyo nafikiria hii inatokana na weledi wangu mzuri wa
uelewa katika taaluma ya matibabu ya michezo, nilimpokea
nikamfanyia vipimo pamoja na matibabu (angalia picha na maelezo ya tiba
hapo chini).
Nimewasaidia wachezaji wa yanga
waliokuwa na shida mbalimbali za kimatibabu hasa yale yaliyokuwa
sugu katika michezo (Hissan) wewe ni shahidi, nina reference ya
Mwashiuya, Juma Abdul na Canavaro pamoja na wachezaj wengine
mbalimbali sijawahi lalamikiwa hata siku moja.
Nilimtibu Kwa muda wa wiki mbili
kwa jeraha la goti na kupona kabisa ,nakumbuka tarehe 3 Februari,
Yanga walicheza dhidi ya Stand United nikiwa nyumbani naangalia
mchezo huo ambao Ngoma aliumia na kushindwa kuendelea na mchezo, baadaye
nikamwandikia sms kwa Whatsap kujiridhisha kama bado jereha
linamsumbua,? akasema, hapana anachoumwa Sasa ni groin ikiwa na
maana kiuno au wengine hupenda kusema nyonga na alinijibu Kwa
whatsap SMS (screen shot nimekutumia), nikamuahidi kumsaidia tena
kwa tatizo hilo,baada ya matibabu akasema anajisikia amepona na
hata majibu ya vipimo hayakuonyesha tatizo (picha za vipimo na
matibabu hizo nimetuma).
Kitaalamu Kuna aina nne ya
matibabu katika mpira, kuna sports medicine doctor, physiotherapy,
sport nutrition advisor na chiropractor ambayo tunaita matibabu
mkandamizo utaalam huu nchi yetu Hakuna, Ngoma aliwaongopea
viongozi wa Yanga SC kwa kuja na report ya kutengenezwa kutoka
London Health ambayo imeandikwa na physiotherapy na siyo
daktari wa Michezo.
Fomu ya FIFA ina sehemu ya daktari
wa timu na daktari wa viungo, daktari wa viungo hawez kuandika
report Ya Mchezaji itakuwa mara ya kwanza Tanzania.
Ukitazama report ya London Health
haiko kwenye maandishi ya kidaktari kabisa inaonekana ilikuwa
mahitaji ya Mgonjwa, report ya Medical ina sehemu tatu, historia
ya mgonjwa ,vipimo na ugonjwa ulioonekana na matibabu
yaliyofanyika ambapo daktari wa mazoezi atachukua report kutoka
Kwa daktari.
Niliwaambia ukweli viongozi wa Yanga SC
na wewe ukiwemo uliponiuliza (Februari 18) juu ya tatizo lake,
nikawajibu kuwa amepona na hana tatizo lolote kiafya hicho ndicho
kilichomkasirisha Ngoma na kuamua kunichafua, ukweli ndio umenifanya
mimi kuchafuliwa.
Sio kitu kizuri kuonyesha report ya
Mgonjwa lakini hamna namna, nataka uma wa wana Yanga na wapenzi wa
mpira waujue ukweli kuhusu Ngoma, Yanga SC wamekuwa wanaleta wagonjwa
kwangu wakati wana daktari wa timu hii inaonyesha ubora wangu
wa kazi na imani waliyonayo kwangu, sio jambo jema kwangu kulikalia
kimya jambo ambalo linahatarisha mustakabali wa taaluma yangu.
Niwaombe radhi wote niliowakwaza kwa
namna moja ama nyingine, nawaomba mliokuwa na imani muendelee kuniamini
na sitowaangusha, imani yenu kwangu isipotee kwa jambo hili.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment