Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Bishop Josephat Gwajima amesema
kuwa Jumatano hii atatembelea Clouds Media Group kwajili ya kuwapa pole
kwa yaliyotokea hivi karibuni.
Ijumaa iliyopita kituo hicho kilivamiwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es
salaam, Paul Makonda akiwa na askari wenye mitutu kitendo kilichopingwa
na wadau mbalimbali wa habari.
“Kesho Tarehe 22/03/2017 saa nne kamili asubuhi, nitatembelea Ofisi za
Clouds Media ili kuwapa pole kwa yaliyotokea.” aliandika mchungaji huyo
kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment