Wakili Peter Kibatala amesema polisi wamepiga picha nyumbani kwa Askofu
waKanisa la Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat
Gwajima.
Kibatala ambaye ni wakili wa Askofu Gwajima amesema jana kuwa mbali na
kupekuwa nakupiga picha kila kona walikwenda katika kanisa lake lililopo
Ubungo.
“Waache wafanye yao na sisi tutafanya yetu kisheria. Kwani hatuwezi
kuwazuia Polisi kufanya shughuli yao na baada ya kumaliza na sisi
tutajua nini cha kufanya,” amesema Kibatala.
Msemaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, David Mngongolwa amesema Gwajima alikwenda jana kuripoti kama alivyoamriwa kufanya hivyo.
Mngongolwa amesema baada ya kuripoti askari walimchukua na kwenda naye
nyumbani kwake wakakaa kwa dakika zisizozidi sita na kuondoka naye.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Suzan Kaganda amesema hana
taarifa za kukamatwa kwa Gwajima kwa maelezo kuwa alikuwa katika kikao.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment