Rais
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameendelea kusisitiza kuwa kuwa
Serikali haitatoa chakula cha msaada kwa watakaopatwa na njaa ilihali
wanaweza kuzalisha chakula katika maeneo yao.
Rais
Magufuli ametoa kauli hiyo leo katika ziara yake mkoani Pwani, wakati
akizungumza na wananchi wa Somanga, Nangurukuru na Mchinga Moja, ikiwa
ni ziara yake katika mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara.
Amepokea kero za wananchi katika maeneo hayo nakuwataka kufanya kazi kwa bidii ikiwemo kuzalisha mazao ya chakula cha kutosha
"Najua
mmezoea kusikia maneno mazuri mazuri kuwa hakuna atakayekufa kwa njaa,
sasa mimi nasema usipofanya kazi, usipolima mazao na kupata chakula
wakati mvua inanyesha Serikali haitatoa chakula cha bure kwa wenye njaa,
ni lazima tufanye kazi, sasa hivi mvua zinanyesha limeni mazao ya
chakula" amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.
Pia
Rais Magufuli amezungumza na wananchi wa Ikwiriri na kupokea kero zao
ambapo amewaagiza Mamlaka ya Maji katika Mji huo kuhakikisha mradi wa
maji uliojengwa na kukamilika tangu mwaka 2015 kwa gharama ya Shilingi
Bilioni 5, unaanza kutoka maji kabla ya mwisho wa Mwezi huu na pia
amepiga marufuku utozaji wa ushuru kwa wafanyabiashara wadogowadogo wa
mazao.
Aidha,
Mhe. Dkt. Magufuli amewaagiza viongozi wa Mkoa wa Lindi kushughulikia
migogoro ya wakulima na wafugaji iliyoanza kuibuka mkoani humo na
ameahidi kutoa Shilingi Milioni 20 kusaidia ujenzi wa Zahanati ya
Somanga.
Mbali
na hayo Rais Magufuli amewaagiza Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Kilwa kujenga kituo cha mabasi cha Nangurukuru na pia amemuagiza Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Lindi kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Mchinga
Mhe. Hamidu Bobali kuhakikisha anapeleka Daktari katika kijiji cha
Mchinga Moja ili kutatua kero ya wananchi kukosa huduma ya matibabu.
Mhe. Rais Magufuli ataendelea na ziara yake kesho tarehe 03 Machi, 2017 hapa Mkoani Lindi
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment