Beki wa Simba Abdi Banda hivi sasa yupo huru kuitumikia klabu yake ya
Simba baada ya leo adhabu yake kutangazwa kumaliza kutumikia adhabu
yake . Mchezaji huyo alifungiwa na Bodi ya Ligi baada ya kumpiga ngumi
mchezaji wa Kagera Sugar, George Kavila
Kamati ya nidhamu ilikaa siku ya jana na wakati inakaa tayari mchezaji
huyo alikuwa amekosa mechi mbili hivyo kamati ilipitia na kusikiliza
pande zote mbili na kufanya maamuzi kuwa zile mechi mbili ambazo
mchezaji huyo alizikosa ndiyo adhabu yake tosha kwa kosa alilofanya.
Awali mchezaji huyo baada ya kufanya tukio hilo ambalo mwamuzi
hakuliona, alisimamishwa kucheza ligi kuu kusubiri maamuzi, na akakosa
michezo dhidi ya Mbao FC na Toto Africans.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment