Msanii wa hip hop kutoka Weusi, Nikki wa Pili, ametia neno katika sakata
linaloendelea la kupigwa marufuku kwa filamu za nje kwa madai
zinaingizwa bila kulipiwa kodi hali ambayo imesababisha kuwa nyingi na
kuzinyima filamu za ndani nafasi ya kufanya vizuri sokoni.
Hatua hiyo imekuja baada ya siku ya Jumatano wiki hii baadhi ya wasanii
wa filamu nchini kuandamana wakiwa na Mkuu wa Mkoa Dar es salaam, Paul
Makonda, kupinga filamu hizo ambapo RC huyo alipiga marufuku filamu hizo
huku akitaka wafanyabishara kufuata taratibu za kuziingiza nchini.
Baadhi ya wasanii wa filamu na muziki wamekuwa wakipingana na hatua hiyo
ambapo Alhamisi hii, rapa Nikki wa Pili ameamua kutia neno kwenye
sakata hilo.
“Nchi zote zilizoendelea zililinda masoko ya nyumbani, ndio tulilinde
lakini wenye movie nao wajilinde kwa kujiongeza kila kukicha,” alitweet
Niki wa Pili.
“Bongo Movies mwanzoni walikuwa na soko, kuanza ni kujaribu, but ku
sustain is a science, mwendelezo wa lolote huitaji maarifa na maisha ya
mwigizaji tofauti na mwanamuziki, Denzel na Jiga tofauti, sasa waigizaji
wanaishi ki bongo fleva,” aliongeza.
Wasani wengine ambao walipinga maandamano hayo ni pamoja na Steve
Nyerere ambaye alikuwa mwenyekiti wa Bongo Movie Unit pamoja na Bella
Fasta.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment