Home »
Habari Moto
» PESA Zazidi Kuvuruga Chama Cha CUF...Lipumba Atinga Mahakani.Fahamu zaidi hapa.
Mgororo wa ruzuku ndani ya Chama cha
Wananchi (CUF) unazidi kupamba moto baada ya mwenyekiti wa chama hicho
anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim
Lipumba kwenda kuitetea mahakamani.
Profesa Lipumba na Mkurugenzi wa Fedha
na Uchumi wa chama hicho, Thomas Malima wamefungua maombi Mahakama Kuu
wakiomba waunganishwe kwenye kesi iliyofunguliwa na Bodi ya Wadhamini wa
CUF, walio upande wa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad.
Katika kesi ya msingi ya ruzuku namba 21
ya mwaka 2017, wadai wanaiomba Mahakama imzuie msajili kutoa ruzuku kwa
CUF na imuamuru Sh360 milioni alizozitoa kwa kina Profesa Lipumba
zirejeshwe kwenye akaunti rasmi ya chama.
Wadaiwa katika kesi hiyo ni Msajili wa
Vyama vya Siasa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, lakini Profesa Lipumba
na Malima wamewasilisha maombi mahakamani nao waunganishwe kwenye kesi
hiyo upande wa wadaiwa.
Maombi hayo yalitajwa jana na Malima
aliieleza mahakama wakiwa viongozi halali wa chama hicho, wanaomba
kujumuishwa kwenye shauri hilo kwa kuwa wana masilahi na shauri hilo.
Wakili wa CUF upande wa Katibu Mkuu,
Juma Nassoro na Wakili wa Serikali, Hang Chang’a waliieleza mahakama
kuwa bado hawajapewa hati za maombi hayo.
Jaji Wilfred Dyansobela aliamuru
waombaji hao (kina Lipumba) kuwapatia nyaraka hizo na amepanga
kusikiliza maombi hayo Juni 6, siku ambayo kesi ya msingi itatajwa.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Related Posts:
Zitto Kabwe Aitaka Serikali Itangaze Balaa la Njaa.Fahamu zaidi hapa.
Kiongozi
wa Chama cha ACT –Wazalendo, Zitto Kabwe ameitaka Serikali kutangaza
rasmi baa la njaa kwa mujibu wa sheria kutokana na hali ya chakula kuwa
mbaya nchini.
Kauli
ya Zitto imetolewa wakati Waziri Mkuu Kassim … Read More
SINGIDA: Basi la Mohammed Trans Lapata Ajali, Watu Kadhaa Wafariki Dunia.Fahamu zaidi hapa.
Nimepita hapa kidogo kabla ya kufika Manyoni nimekutana na hii ajali
mbaya. Inadaiwa watu 3 wamefariki na majeruhi ni 6. Aidha, inasemekana
ni walimu ambao walilikodi basi kutoka Tanga.
Chanzo cha ajali ni gari ndogo lil… Read More
Magari yenye taa za mwanga mkali yapigwa marufuku.Fahamu zaidi hapa.
POLISI
Kikosi cha Usalama Barabarani kimesema kitaanza kukamata magari yote
ambayo yamewekwa taa zenye mwanga mkali (spotlights) kwa kuwa uwekaji wa
taa hizo, ni kinyume na sheria ya usalama barabarani.
Uwekaji
wa t… Read More
Serikali Inawajibika Kumtafuta Ben Saanane – Lissu.Fahamu zaidi hapa.
MWANASHERIA Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu
Lissu, amesema serikali ndiyo yenye wajibu wa kumtafuta na kumpata raia
wake, Ben Saanane, ambaye amepotea kwa miezi ipatayo miwili sasa.
Liss… Read More
Lowassa, Maalim Seif Kutikisa Zanzibar Kesho.Fahamu zaidi hapa.
Wanasiasa
wakongwe nchini, Maalim Seif Sharif Hamad aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa
Rais wa Zanzibar na Edward Lowassa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania katika, kesho wanatarajia kuungana kwa mara y… Read More
0 comments:
Post a Comment