Walioshuhudia
mashambulizi hayo wanasema watu tisini na saba wameuawa siku ya Jumatano katika
kijiji cha Kukawa kilichopo karibu na Ziwa Chad.
Habari
zinasema pia wanaume 48 wamepigwa risasi na wapiganaji katika mashambulizi
tofauti siku ya Jumanne.
Mashuhuda
wanaokimbia eneo lililopo karibu na Ziwa Chad wanasema idadi kubwa ya
wapiganaji wamevamia vijiji vitatu ambapo wameuwa wanaume, wanawake na watoto.
Baadhi
ya ripoti zinasema walipigwa risasi huku wengine wakielezea jinsi wapiganaji
hao walivyowachinja watu na kuchoma majengo.
Upande
wa Kusini, nje kidogo na mji wa Monguno, kundi la wapiganaji wa Boko Haram
wamefika usiku wakati watu walipokuwa wanaswali. Waliwasubiri mpaka
walipomaliza kuswali na kuwatenganisha wanaume na wanawake na baadae kuanza
kuwamiminia risasi wanaume.
Mwanasiasa
anayewakilisha eneo hilo, Mohammed Tahir amesema awali alitoa tahadhari kwa
jeshi la Nigeria kwamba vijiji hivyo viko hatarini kwa sababu Boko Haram
wameweka makazi katika maeneo hayo baada ya kutimuliwa katika himaya yao ya
msitu wa Sambisa.
Haya
ni mashambulizi mabaya zaidi kufanywa na Boko Haram katika kipindi cha wiki
kadhaa.
Kundi
hilo limekuwa likilipuwa mabomu kadhaa baada ya kudhoofishwa na majeshi ya
Nigeria.
Rais
wa Nigeria, Muhammadu Buhari amesema kipaumbele chake ni kuimarisha mapambano
dhidi ya Boko Haram.
0 comments:
Post a Comment