Uongozi
wa klabu ya Yanga, umeandika barua kuomba kuutumia Uwanja wa Amaan
mjini Zanzibar kwa ajili ya mechi zake za Ligi Kuu Bara na mashindano
mengine.
Yanga
imechukua uamuzi huo baada ya Serikali kutangaza kuifungia yenyewe
pamoja na Simba kuutumia Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Serikali imetangaza kuufungia uwanja huo baada ya vurugu za mashabiki zilizojitokeza wakati wa mechi ya watani hao.
Uamuzi
huo wa Yanga kama utapita kupitia ombi lao, maana yake timu
zitalazimika kusafiri kwenda Zanzibar kuifuata Yanga ambayo itakuwa
nyumbani.
0 comments:
Post a Comment