Serikali
ya Tanzania na nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC),
wametiliana saini makubaliano ya kuimarisha ushirikiano wao katika
nyanja mbalimbali ikiwemo suala la ulinzi na usalama pamoja uchimbaji wa
mafuta katika ziwa Tanganyika.
Akiongea
leo Ikulu Jijini Dar es Salaam mara baada ya kufanya mazungumzo na Rais
Joseph Kabila, Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa
pamoja na mambo mengine wamekubaliana ushirikiano wa kimaendeleo katika
uwekezaji pamoja na jinsi ya kusimamia uchaguzi ujao wa nchi hiyo
kupitia uongozi wake katika nchi za Jumuiya ya nchi za SADC.
Aidha
Rais Magufuli amesema kuwa mbali ya kuangalia masuala ya kiusalama
nchini humo pia amemuomba wafanyabiashara kutoka nchini Congo kuja
kuwekeza nchini pamoja kutumia bandari ya Dar es Salaam kwa katika
usafirishaji wa bidhaa.
Rais
Magufuli amesema kuwa wamekubaliana na mamlaka ya bandari kuongeza muda
wa mizigo inayokaa bandarini mpaka muda wa siku 30 badala ya siku 14
kama ilivyo awali huku akiongeza kwa kusema kuwa hata ujenzi wa reli ya
Standard Geuge utaifaidisha Congo katika usafirishaji wa mizigo.
0 comments:
Post a Comment