Saturday 18 February 2017

Baada ya Sekeseke la Madawa ya Kulevya Kutulia,TID Aamua Kumtaja Tena Diamond..!!!..Fahamu zaidi hapa.

Kwa sasa msanii TID Mnyama anahakikisha anarudisha makali yake ya zamani kwenye muziki. Muimbaji huyo amewaahidi mashabiki wake kufanya kazi na Diamond hivi karibuni.
Akiongea kwenye kipindi cha XXL, kupitia Clouds FM Ijumaa hii, Mnyama amesema kuna nyimbo anayofikiria kumshirikisha Diamond ambaye taarifa hizo tayari ameshazipata.
“Nina ngoma nafikiri itafaa zaidi nikimshirikisha Diamond. Diamond ameshapata habari nafikiri tutaifanya ngoma hiyo soon as possible,” amesema TID.
Kwa sasa msanii huyo ameachia wimbo wake mpya aliomshirikisha rapper Fid Q unaojulikana kama ‘Maisha ya Jela’ pamoja na mwingine uitwao Woman.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment