Monday 27 February 2017

Kichuya supper Sub hatari mbayo akiingia tu afanyi makosa.Fahamu zaidi hapa.

WINGA Shiza Ramadhani Kichuya, kwa mara nyingine tena siku ya Jumamosi  aliibuka shujaa wa Wekundu wa Msimbazi baada ya kutokea benchi na kuisaidia Simba kushinda 2-1 dhidi ya mahasimu, Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Kichuya aliyempokea beki Novatus Lufunga dakika ya 55, kwanza alimsetia mshambuliaji Mrundi, Laudit Mavugo kuifungia bao la kusawazisha Simba dakika ya 66 kabla ya yeye mwenyewe kufunga la ushindi dakika ya 81.

Ikumbukwe Kichuya ndiye aliyeifungia Simba bao la kusawazisha dakika ya 86 Oktoba 1, mwaka jana timu hizo zikitoka sare ya 1-1 baada ya Amissi Tambwe kutangulia kuifungia Yanga dakika ya 26 kwa makosa ya Lufunga tena.

Yanga SC walitangulia kwa bao la mapema tu dakika ya tano la Simon Msuva kwa mkwaju wa penalti, baada ya kiungo Mzambia, Obrey Chirwa kuangushwa kwenye boksi na Lufunga.
 Obrey Chirwa akimtoka beki Novaty Lufunga leo kabla ya kuangushwa na kusababisha penalti
 Laudit Mavugo akimiliki mpira mbele ya beki wa Yanga, Kevin Yondan.
 Haruna Niyonzima akigombea mpira na Janvier Bokungu.
Amissi Tambwe akiwa chini baada ya kugongana na Lufunga

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa


0 comments:

Post a Comment