Monday 20 February 2017

Wolper Afunguka Kulewa Pati ya Mtoto wa Diamond..Nillan.Fahamu zaidi hapa.

BAADA ya kuwa ‘topic’ kwenye sherehe ya 40 ya mtoto wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Nillan iliyofanyika hivi karibuni, Muigizaji Jacqueline Wolper  ameibuka na kusema katika maisha yake yote hajawahi kulewa.
Licha ya kuonekana kupoteza balansi hadi kufi kia hatua ya kutaka kuanguka alipokuwa akiwachana watu wanaomponda wifi  yake, Zarinah Hassan Zari ‘The Boss Hassan Zari ‘The Boss Lady’ kiasi cha watu kuamini hata maneno yaliyomtoka hakuyadhamiria bali ni pombe, Wolper alisema siku hiyo hakuwa amelewa na alichokiongea alimaanisha.
“Japo nakunywa lakini siku ile sikulewa na sijawahi kulewa. Niliyoyasema pale nilidhamiria maana watu wamekuwa wakimponda Zari kwa kuedit picha zake kitu ambacho si cha kweli na mimi lazima nimtetee yule ni mke wa bosi wa mume wangu,” alisema Wolper


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment