Friday 24 February 2017

Dr Harrison Mwakyembe Aonywa na Chama cha Wanasheria Afrika Mashariki.Fahamu zaidi hapa.

Chama cha Wanasheria Afrika Mashariki (EALS) kimemwandikia barua Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe kikimtaka aache kuingilia uchaguzi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).

Barua hiyo imekuja baada ya Dkt. Mwakyembe kudaiwa hivi karibuni kutishia kuifuta TLS kwa madai kwamba imeanza kuingiliwa kisiasa.

Barua hiyo iliyoandikwa na kusainiwa na Rais wa EALS, Richard Mugisha, inasema TLS si chama cha kisiasa na kimeanzishwa kwa kufuata sheria zote.

“Mheshimiwa Waziri, tumesikitishwa na taarifa ambazo zimeenea kwenye vyombo vyote vya habari na gazeti la East African la Februari 18 ambalo limekunukuu ukisema kwamba Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) kina muingiliano wa kisiasa,” inasema sehemu ya barua hiyo.

Katika barua hiyo, Mugisha anasema wanasheria wanatakiwa wapewe uhuru, wasiingiliwe na serikali kama ilivyo kwa nchi nyingine kwani kuingilia ni sawa na kuvunja sheria za nchi.

Rais wa sasa wa TLS, John Seka amesema kuwa chama chake kimefurahishwa na barua hiyo kwa Waziri na kwamba nao pia wanafanya taratibu kumuona ili kujadili mustakabali wa chama hicho.

Alisema kuwa TLS inaendelea na mchakato wa uchaguzi kama ulivyopangwa na kuwataka wagombea wote kujiandaa kwa uchaguzi huo ambao alisema ni halali.

Uchaguzi wa chama hicho unatarajiwa kufanyika machi 18 mwaka huu, huku wagombea kutoka vyama vya upinzani wakiwa wamejitokeza kuwania nafasi ya uongozi wa juu.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa


0 comments:

Post a Comment