Thursday, 9 June 2016

#BURUDANI>>>>Drake Avunja Rekodi hii, ambayo ilivunjwa na 50 Cent Miaka kadhaa iliyopitaFahamu zaidi hapa.

Hakuna rekodi ngumu kuvunja kama rekodi ya kuwa na nyimbo bora ikishikilia namba moja kwenye chati za billboard na wakati huo huuo uwe na album bora nayo ipo namba moja kwenye chati za  billboard kitu ambacho amewahi kufanya rapa 50 Cent na sasa ni zamu ya Drake.


Baada ya Drake kuvunja rekodi ya Eminem kwa kukaa na album yake namba moja kwa zaidi ya wiki tani sasa Amevunja rekodi ya 50 kwa kuwa na wimbo nambo moja kwenye Billboard  Top 100 ambao ni ‘One Dance’ Ft Wizkid na Kyla na album yake ya VIEWS ni namba moja kwenye Billboard hot 200.

50 Cent alifanya hivi mwaka 2005 kupitia wimbo wa “Candy Shop” na album ya The Massacre na zilikaa namba moja kwa wiki sita mfululizo. Hakuna msanii wa kiume kafikia hii bado.

Kwa upande wa wasanii wa kike ni Adele aliyekaa wiki sita na wimbo wa “Hello” na album yake ya 25 ilikuwa mwezi December kulelekea January.

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment