Mchezaji wa wa mchezo wa tenisi,Maria Sharapova, amesimamishwa kushiriki katika mchezo huo kwa miaka miwili mfululizo, hatua hiyo imekuja baada ya nyota huyo kufanyiwa vipimo vya kugundua kama anatumia dawa za kusisimua misuli na kukutwa ni mtumizi wa dawa aina ya, Meldonium. Nyota huyo mwenye miaka ishirini na tisa aliandika katika ukurasa wake wa facebook kwamba atakata rufaa kwa kile alichokiita uamuzi mkali na isivyo haki kutoka katika shirikisho hilo la kimataifa la mchezo wa tenisi.
Sharapova mwanzoni mwa mwaka huu alipigwa marufuku ingine mwezi March, wakati ilipotangazwa kwamba hataweza kufanyiwa vipimo hivyo vya kiuchunguzi wakati michuano ya Australian Open ilipokuwa inajiri mwezi January.
Akijitetea kuhusiana na matumizi ya dawa hiyo aina ya Meldonium ameeleza kwamba ni kwasababu za kitabibu ndipo alitumia dawa hizo.
Jina la Maria Sharapova ameshaandikwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Urusi watakao kwenda kwenye michuano ya kufukuza upepo ya Rio Olympic mwezi August .
Marufuku hiyo imeanza kutekelezwa tangu January 26,2016.
Source: BBC
0 comments:
Post a Comment